Nenda kwa yaliyomo

Kigusii

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Ekegusii)

Kigusii ni lugha ya Kibantu nchini Kenya inayozungumzwa na Wakisii. Mwaka wa 2009 idadi ya wasemaji wa Kigusii imehesabiwa kuwa watu 2,205,000. Pia kuna wasemaji 300 tu nchini Tanzania. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kigusii iko katika kundi la E40. Hasa Kigusii huzungumzwa eneo la Kisii ambalo makao yake makuu ni Mji wa Kisii (kati ya Ziwa Victoria na mpaka wa Kenya-Tanzania) katika Mkoa wa Nyanza.

Kigusii imeainishwa kama lugha ya Bantu ya Kati, kundi moja na Lugha ya Kikuria, kundi ambalo limepewa anwani ya E.10 katika makala ya Aina za Lugha za Bantu yaliyotungwa na Malcolm Guthrie. Lugha zinazofanana zinapatikana nchini Tanzania nazo ni:

Sauti za Gusii takribani zote zinaambatana na irabu.

Lugha ya Kisii ina irabu saba, zingine zikiundwa kutokana na urefu wa kuzitamka. Kwa mfano, maneno 'bora' (kosekana) na 'boora' (sema) yanatofautishwa tu na urefu wa irabu 'o' n 'oo'.

Irabu za Kisauti kwa Lugha ya Gusii
. Mbele Kati Nyuma
Iliyofungwa i u
Karibu-Iliyofungwa ɪ ʊ
Kati-Wazi ɛ ɔ
Wazi a

Konsonanti

[hariri | hariri chanzo]

Katika jedwali lifuatalo, alama za uandishi ambazo hutofautiana na zile za Alfabeti ya Kimataifa (IPA) zimewekewa mabano. palipo na alama mbili pamoja, ya kulia inaashiria konsonanti inavyotamkwa.

Sauti za Konsonanti katika Lugha ya Kisii, kulingana na IPA.
. bilabial alveo-palatal palatal velar
plosive p   b t c (c) k   g
fricative   s    
affricate     cç (c)  
nasal m n ɲ (ny) ŋ (ng')
trill   r    
approximant w   j (y)  

Mofolojia ifuatayo pia inatumika:

  • n+r = nd
  • n+b = mb
  • n+g = ŋg
  • n+k = ŋk
  • n+m = mm

Bickmore, Lee

  • 1997. Problems in constraining High tone spread in Ekegusii. Lingua, Toleo la 102, uk. 265-290.
  • 1998. Metathesis and Dahl’s Law in Ekegusii. Studies in the Linguistic Sciences, Toleo la. 28:2, uk. 149-168.
  • 1999. High Tone Spreading in Ekegusii Revisited: An Optimality Theoretic Account. Lingua, toleo. 109, uk. 109-153.

Cammenga, Jelle

  • 2002 Phonology and morphology of Ekegusii: a Bantu language of Kenya. Köln: Rüdiger Köppe Verlag.

Whiteley, Wilfred H.

  • 1956 A practical introduction to Gusii. Dar es Salaam/Nairobi/Kampala: East African Literature Bureau.
  • 1960 The tense system of Gusii. Kampala: East African Institute of Social Research.
  • 1974 Language in Kenia. Nairobi: Oxford University Press.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]

Kusikiza

[hariri | hariri chanzo]

Tazama Pia

[hariri | hariri chanzo]