Dura ya maji
Mandhari
Dura ya maji (en:water cycle) ni jinsi gani maji huzunguka duniani kuanzia uso wa ardhi, angani hadi uso wa ardhi tena na chini ya ardhi. Maji huzunguka kwa kutumia michakato wa uvukizaji na usimbishaji.
Dura
[hariri | hariri chanzo]- Kwanza maji yaliyopo kwenye uso wa ardhi huvukiza. Maana yake miale ya jua inapashia joto maji kwenye nchi kavu au baharini na maji hayo hubadilika kuwa mvuke ambao ni mwepesi na kupanda juu kwenye angahewa.
- Mvuke wa maji unaingia katika akiba kubwa ya maji kwenye angahewa; kutegemeana na halijoto ya hewa maji hukaa huko kama gesi au yanaendelea kujikaza kuwa mawingu.
- Wakati mawingu hupoa zaidi mvuke unaendelea kujikaza na kutonyesha.
- Hapa usimbishaji unaanza na maji huanguka chini kwa umbo la mvua au theluji.
- Mvua hugonga uso wa ardhi. Sehemu inapita juu ya uso wa ardhi kwenye mito moja kwa moja. Sehemu nyingine inaingia katika udongo wa ardhi. Kutoka hapo italisha chemchemi.
- Kutoka chemchemi maji hutokea kwa umbo la mito na vijito,
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Dura ya maji kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |