Donashano Malama
Donashano Malama (alizaliwa 1 Septemba , 1991) ni mchezaji wa soka wa Zambia ambaye anachezea katika klabu ya Chippa United F.C. na timu ya taifa ya mpira wa miguu ya Zambia.
Kazi ya klabu
[hariri | hariri chanzo]Mnamo Januari 2018, Malama alisaini katika klabu ya Botola baada ya kumalizika kwa mkataba wake katika klabu ya Nkana nchini zambia.
Chippa United F.C.
[hariri | hariri chanzo]Mnamo Januari 2019, Malama alihamia upande waAfrika Kusini katika klabu ya Chippa United F.C., akisaini mkataba pamoja na Bangaly Keita.
Alicheza mchezo wake wa kwanza wa ligi mnamo 3 Februari 2019, akiingia kama mbadala dakika ya 66 wa Repo Malepe kwenye mchezo ambao walitoka sare ya 1-1 dhidi ya Baroka F.C ..
Kazi ya kimataifa
[hariri | hariri chanzo]Malama alicheza kwa mara ya kwanza katika timu ya taifa mnamo tarehe 28 Aprili 2013 katika ushindi wa 2-0 dhidi ya timu ya taifa ya Zimbabwe.
Alikuwa sehemu ya kikosi cha Zambia kilichoshiriki Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2015, na alicheza kwenye mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi dhidi ya Cape Verde akiingia kama mbadala.
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Donashano Malama kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |