Don Riddell

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Don Riddell (amezaliwa 7 Septemba 1972 mjini Edinburgh, Uingereza) ni mtangazaji wa habari wa kutoka Uingereza na aliwahi kuwa mwandishi wa habari za michezo. Yeye alikuwa mtangazaji mmoja kati ya wanne wa CNN mjini London waliokuwa wakitangaza habari za World Sport ; pia aliwahi kutangaza taarifa za CNN za Living Golf. Hivi sasa yeye ni mmoja wa watangazaji wa kipindi cha asubuhi cha Ulaya kiitwacho CNN Today .

Riddell alijiunga na CNN mwaka 2002. Awali alikuwa akifanya kazi katika London News Network, ambako alifanya kazi kama mtangazaji wa michezo kwa kipindi cha London Tonight . Alianza kazi yake ya kuripoti katika mikoa ya Uingereza.

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Riddell alihudhuria Chuo Kikuu cha Leeds na kufuzu kwa shahada ya Uandishi habari / Mawasiliano na Masomo ya Utamaduni.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]