Nenda kwa yaliyomo

Djihad Bizimana

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Djihad Bizimana (alizaliwa 12 Desemba 1996) ni mchezaji wa mpira wa miguu wa Rwanda ambaye anacheza kama kiungo mkabaji wa klabu ya Waasland-Beveren katika ligi Daraja la Kwanza nchini Ubelgiji na timu ya taifa ya Rwanda.

Kazi ya klabu

[hariri | hariri chanzo]

Bizimana ni moja ya vijana wa klabu ya Etincelles tangu akiwa na umri wa miaka 15, na alianza kazi yake na klabu ya Rayon.

Mnamo tarehe 26 Aprili, 2018, Bizimana alijiunga na klabu ya Waasland-Beveren kutoka katika klabu ya APR ya Rwanda.Bizimana alianza mazoezi yake ya kwanza katika klabu hiyo ya Waasland-Beveren katika mchezo wa kwanza ambao walitoka sare ya 2-2 na S.V. Zulte Waregem tarehe 28 Julai 2018.


Kazi ya kimataifa

[hariri | hariri chanzo]

Bizimana ni mchezaji wa timu ya taifa ya Rwanda. Bizimana alichaguliwa katika timu ya taifa ya mpira wa miguu ya Rwanda katika mechi waliyofungwa 2-0 na timu ya taifa ya Zambia mnamo 29 Mei 2015.


Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Djihad Bizimana kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.