Diogo Jota
Diogo José Teixeira da Silva, anajulikana kama Diogo Jota, alizaliwa 4 Desemba 1996 ni mchezaji wa soka wa Ureno ambaye anacheza katika klabu iiliyopo katika ligi kuu ya Uingereza iitwayo Wolverhampton Wanderers.
Kazi ya klabu
[hariri | hariri chanzo]Atlético Madrid
[hariri | hariri chanzo]Mnamo 14 Machi 2016, Jota alikubali mkataba wa miaka mitano akiwa na klabuya Atletico Madrid .Mnamo 26 Agosti alirudi katika nchi yake na kujiunga na klabu ya FC Porto kwa mkopo wa mwaka mmoja. Mnamo 1 Oktoba alifunga goli la kwanza katika ushindi wa 4-0 dhidi ya C.D. Nacional.
Wolverhampton Wanderers
[hariri | hariri chanzo]Mnamo 25 Julai 2017, Jota alihamia katika klabu iiliyopo nchini Uingereza iitwayo Wolverhampton Wanderers kwa mkopo wa muda mrefu.Alifunga goli lake la kwanza 15 Agosti, ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya Hull City.
Mnamo 30 Januari 2018, ilitangazwa kuwa katika mpango wa kudumu katika klabu ya Wolverhampton Wanderer. Alifunga magoli 17 bora katika mwaka wake wa kwanza.
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Diogo Jota kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |