Nenda kwa yaliyomo

Dido

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Shujaa wa Trojan Aeneas anamwambia Dido kuhusu Trojan War (Guérin, 1815). Katika Aeneid Dido anampenda Aenea na anavunjika moyo anapoondoka.

Dido (au Elissa, kwa lugha ya Kigiriki na Kilatini) alikuwa mwanzilishi na malkia wa kwanza wa mji-milki wa Kifinisia wa Karthago (uliyopo Tunisia), mwaka 814 KK. Kulingana na hadithi, yeye alikuwa malkia wa mji-milki wa Finisia wa Tiro [1]uliyopo Lebanon) ambaye alikimbia utawala wa kikatili ili kuanzisha mji wake mwenyewe katika Afrika Kaskazini Magharibi. Taarifa kuhusu Dido inatokana na vyanzo vya Kigiriki na Kirumi vya zamani, vyote vikiandikwa baada ya kuanzishwa kwa Kartago, hivyo ukweli wake bado haujathibitishwa. Marejeo ya kale kuhusu Dido yanadaiwa kuwa ya Timaeus, aliyekuwa akifanya kazi karibu na mwaka 300 KK, takribani karne tano baada ya tarehe inayotolewa kwa kuanzishwa kwa Kartago.

Maelezo kuhusu tabia, maisha, na jukumu la Dido katika kuanzisha Kartago yanajulikana zaidi kupitia hadithi iliyotolewa katika mashairi ya Kiroma ya Aeneid, iliyoandikwa karibu mwaka wa 20 KK, ambayo inaeleza hadithi ya kihistoria ya shujaa wa Troia, Aeneas. Dido anaelezwa kama mwanamke mwerevu na mjasiriamali ambaye alikimbia ndugu yake mkatili na dikteta, Pygmalion, baada ya kugundua kwamba alikuwa na jukumu katika kifo cha mumewe. Kupitia busara na uongozi wake, mji wa Kartago ulianzishwa na kufanikiwa.

Dido bado ni mtu maarufu katika tamaduni na sanaa za Magharibi tangu Renaissance mapema hadi karne ya 21. Katika karne ya 20, aliteuliwa pia kama alama ya kitaifa katika uzalendo wa Tunisia, hivyo wanawake wa Tunisia wanaweza kufafanuliwa kwa mfano wa kishairi kama "Watoto wa Dido".

Dido (Elissa) pia amewahi kuwakilishwa kwenye sarafu ya Tunisia mnamo mwaka wa 2006.[2]

  1. "Elissa – Dido Legend of Carthage". www.phoenician.org. Iliwekwa mnamo 2017-04-14.
  2. Masri, Safwan M. (2017). "Carthage". Tunisia: An Arab Anomaly. Columbia University Press. ku. 93–107. doi:10.7312/masr17950. ISBN 978-0-231-54502-0. JSTOR 10.7312/masr17950.13.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Dido kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.