Delron Buckley
Delron Sebastian Buckley (alizaliwa 7 Desemba 1977) ni mchezaji wa zamani wa kitaalamu wa mpira wa miguu kutoka Afrika Kusini. Nafasi yake ya kupendelea ilikuwa kama winga wa kushoto ingawa pia alikuwa anaweza kucheza kama mshambuliaji. Mnamo Septemba 2021, aliteuliwa kuwa Kocha Mkuu wa timu ya soka ya Chuo Kikuu cha KwaZulu-Natal.
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Alizaliwa Durban, Buckley alianza kazi ya soka na timu yake ya Rovers Durban. Akiwa na umri wa miaka 17, alisainiwa na klabu ya Ujerumani ya VfL Bochum. Buckley alipitisha sehemu kubwa ya kazi yake nchini Ujerumani, akicheza katika timu za vijana ya Bochum na kuanza kucheza mpira na Bundesliga mnamo 1995. Buckley hatimaye aliaminikaa kwenye kikosi cha kwanza mwaka 1998 na alikuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha kwanza.
Baada ya kusheherekea misimu tisa ya kitaalamu na Bochum, Buckley aliondoka mnamo 2004 na kujiunga na Arminia Bielefeld ambapo alifurahia msimu wake wenye mafanikio zaidi binafsi, akifunga mabao 15 na kusaidia timu kuepuka kushushwa daraja.Buckley alivutia kusajiliwa na vilabu vingi. Baada ya msimu mmoja tu Bielefeld, Buckley alijiunga na Borussia Dortmund kwa ada ya uhamisho iliyoripotiwa kuwa € 425,000, na kusaini mkataba wa miaka minne.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Delron Buckley kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |