Nenda kwa yaliyomo

Dekkani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Maeneo ya Dekkani
Nyumba za miamba ya itale ni sifa ya kawaida katika mazingira ya Dekkani. Hizi ziko karibu na Hyderabad katika Jimbo la Telangana

Dekkani (kwa Kiingereza: Deccan) ni tambarare kubwa ya juu inayojumisha sehemu kubwa ya Uhindi Kusini.

Tambarare hii inaenea katika majimbo manane ya Uhindi (Telangana, Maharashtra, Andhra Pradesh, Karnataka, Kerala na Kitamil Nadu).

Maeneo yake kwa jumla ni zaidi ya km² 422,000 ambazo ni sawa na asilimia 43 za Uhindi wote.[1]

Umbo la Dekkani ni takriban kama pembetatu; kwa pande mbili kuna bahari na upande wa kaskazini Bara Hindi inaendelea kwenye nchi kavu. Upande wa magharibi milima ya Ghat ya Magharibi inatenga tambarare ya juu na bahari, upande wa mashariki ni safu ya Ghat ya Mashariki. Sehemu hizi za milima huinuka kutoka katika nchi tambarare za pwani hukutana katika ncha ya kusini ya Uhindi. Mpaka wa kaskazini wa pembetatu unafanywa na milima ya Satpura na milima ya Vindhya. Milima hiyo hutenganisha Dekkani na watu wake na kaskazini ya nchi.

Asili ya jina

[hariri | hariri chanzo]

Asili ya jina "dekkani" iko katika neno la kienyeji linalomaanisha "kusini" [2] [3]

  1. Encyc Brit.
  2. Monier-Williams Sanskrit-English Dictionary, p. 498 (scanned image at SriPedia Initiative): Sanskrit dakṣiṇa meaning 'right', 'southern'.
  3. "Deccan | plateau, India". Encyclopedia Britannica (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-03-22.
Makala hii kuhusu maeneo ya Uhindi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Dekkani kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.