David Dobrik

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
David Dobrik

David Julian Dobrik (alizaliwa Kosice, 23 Julai 1996) ni mchekeshaji wa mtandao nchini Slovakia.

Alianza taaluma yake kwenye tovuni ya video inayoitwa Vine halafu alitengeneza kituo cha Youtube kwenye mwaka 2014. Kama ya mwaka 2019, Dobrik anajuliwa kama kiongozi wa kikundi maarufu kinachoitwa The Vlog Squad kinachonyeshwa mara nyingi kwenye vlog zake na kinahusisha rafiki zake mbalimbali. Kama ya Desemba 2019, kituo cha vlog zake kilipokea wanachama millioni 1.5 na vlog zake zilitazamwa mara billioni 6.4. Kituo chake kilikuwa na cheo cha tano kwa vituo vya Youtube kwenye mwaka 2019, mwaka ambao kituo chake kilitazamwa mara billioni 2.4.

Zaidi ya burudani ya mtandao, Dobrik aliigiza na sauti yake kwenye filamu inayoitwa The Angry Birds Movie 2 kama mhusika Axel na, kama ya Desemba 2019, Dobrik ni jaji ya kipindi cha Nickelodeon TV kinachoitwa America’s Most Musical Family.

Maisha ya zamani[hariri | hariri chanzo]

Dobrik alizaliwa Slovakia. Familia yake ilihamia mji wa Vernon Hills, jimbo la Illinois, nchi ya Marekani Dobrik nilipokuwa na miaka sita. Alisomea Vernon Hills High School na alicheza tenisi pale pia. Alipokea cheo cha tatu kwenye mashindano ya tenisi kwa jimbo la Illinois kwenye mwaka 2014. Baada ya kumaliza shule ya sekondari, alihamia mji wa Los Angeles kufuata taaluma yake ya Vine.

Taaluma[hariri | hariri chanzo]

013-2016: Vine na mwanzo wa Youtube[hariri | hariri chanzo]

Kwenye mwaka 2013, Dobrik alitengeneza Vine yake ya kwanza. Alishirikiana na waumbaji wa Vine maarufu wengine kama Liza Koshy, Gabbie Hanna, Jason Nash, na Zane & Heath. Kabla ya kutengeneza kituo cha Youtube chake, Dobrik alishiriki kwenye kikundi cha Youtube kinachoitwa Second Class. Mwishoni mwa kituo hicho kwenye mwaka 2015, Dobrik na wenzake wamepokea zaidi ya wanachama 18,000. Dobrik alitengeneza kituo kibinafsi cha Youtube, David Dobrik, kwenye mwaka 2015. Tangu mwanza wa kituo hicho, video za kituo chake zimekuwa vlog za kuchekesha zinazozingatia hali za maisha ya kweli na maonyesho madogo na wenzake wa Vine. Kwenye mwezi wa nane mwaka 2016, Dobrik alitengeneza kituo cha pili, David Dobrik Too. Anatumia kituo hicho kushiriki makosa yake, video za mashindano, na kukuza ufadhili wake.

2017-Sasa: Taaluma ya Youtube[hariri | hariri chanzo]

Dobrik alipokea washabiki hivi karibuni kwa sababu ya video zake zinazohusisha utani wa binafsi, wanyama wanaopendeza, nyota za Vine na Youtube, watu mashuhuri, na wahusika wa kuchekesha. Zamani, Dobrik alizituma video zake mara tatu kwa wiki lakini sasa ni mara mbili kwa wiki. Anayo podcast inayoitwa ‘VIEWS’ na mtu mashuhuri wa Youtube, Jason Nash. Mara kwa mara, podcast hiyo itawahusisha Joe Vulpis na Natalie Mariduena.

Kwenye Desemba 2018, Dobrik alipewa kwa Youtube tuzo inayoitwa Diamond Play Button kwa sababu kituo chake kilipita wanachama millioni kumi. Dobrik aliitwa mmoja wa ’10 nyota za Mtandao wa Kijamii’ kwa mwaka 2018 kwa gazetti ya PAPER, pamoja na Trisha Paytas na Jaboukie Young-White na wengine.

Kwenye Julai 2019, Dobrik alihusishwa kwa gazetti ya W pamoja na Diana Silvers, Gigi Hadid, na Joe Jonas, kando na wengine, kwa sababu alianzisha akaunti nyingine ya Instagram kwa ajili ya kutumia kamera za zamani. Pia, Dobrik alikuwa jaji kwa mashinadano ya muziki yanayoitwa ‘America’s Most Musical Family’, kando ya Ciara na Debbie Gibson.

Kwenye Agosti 2019, Dobrik alionyeshwa kwa gazetti ya Variety kwenye orodha yao ya ‘Power of Young Hollywood’, kando na watu maarufu kama Blackpink, Billie Eilish, Tom Holland, na Lil Nas X. Kwenye mwezi huo huo, Dobrik alikaribisha sherehe inayoitwa 2019 Teen Choice Awards pamoja na Lucy Hale. Alipokea tuzo ya Choice Male Web Star pia. Dobrik alishiriki na mara ya kwanza kwamba Nickelodeon ilikuwa na mashindano yanayoitwa Kids’ Choice Sports Championship, pamoja na Rob Gronkowski, Lindsey Vonn, Kel Mitchell, na watu mashuhuri wengine.

Kwenye Oktoba 2019, Dobrik alitajwa mtu wa mtandano bora kufuata kwa mtandao wa kijamii kwa vijana kwa kulingana na utafiti wa Piper Jaffray & Co., kando na Kylie Jenner, Donald Trump, LeBron James, na Dwayne ‘The Rock’ Johnson.

Kwenye Novemba 2019, gazeti ya People alimtaja Dobrik ‘Mtu wa Kuvutia Bora Kuliko Wote wa 2019’, juu ya Harry Styles na Shawn Mendes. Mwezi huo huo, Dobrik aliwasilisha tuzo za American Music Awards of 2019, na pia alikuwa jaji kwa sehemu ya kwanza ya Chopped Junior kwa majira tisa.

Kwenye Desemba 2019, Dobrik alitajwa kwa Youtube Rewind 2019 kama mwigizaji wa tano kwa mwaka 2019 kwa sababu video zake zilitazamwa mara billioni 2.4. Pia kwenye mwezi huo huo, video ya Dobrik kwa TikTok iliyohusisha jaribio la ‘elephant’s toothpaste’ ilitajwa Video Bora Kuliko Zote kwa TikTok kwenye 2019. Ilitazamwa mara millioni 180 na watu millioni 17.5 waliipenda video hio.

Kwenye Januari 2020, Dobrik alianzisha app yake ya camera za rununu inayoitwa ‘David’s Disposable’. Inawaruhusu watumiaji kutengeneza picha zinazofanana picha za zamani. App hiyo imenunuliwa zaidi ya mara milioni na pia kwa muda mfupi app bure iliyokuwa maraufu zaidi ya app bure zote, mbali ya Disney+ na Instagram. Ilishinda nafasi kwenye orodha ya kampuni Apple, ‘Apps We Love Right Now’ (‘Apps Tunazipenda Sasa’).

Dobrik pia alikaribishwa na Jimmy Fallon kwa tamthilio yake ‘The Tonight Show’. Ilikuwa mara ya kwanza ya Dobrik kualikizwa kwa televesheni ya usiku. Aliongea kuhusu msukumo wake wa video zake na kituo chake cha Youtube na alizungumzana na Justin Bieber kwa mara ya kwanza. Mwonekano wa Dobrik kwa ‘The Tonight Show’ na Jimmy Fallon kando ya Martin Short na Yola ulionwa kama sababu sehemu hio hio ilitazamwa zaidi ya zote ya wiki hio hio. Miingiliano ya sehemu hio kwenye Facebook, Instagram, na Twitter ilipitia wastani ya sehemu za ‘The Tonight Show’ zaidi ya asilimia 582, kwa kulingana na Nielsen Social Content Ratings.

Kwenye Aprili 2020, Dobrik alitajwa mwigizaji wa kwanza wa Youtube kwa mara ya pili, kwa kulingana na utafiti wa Piper Jaffray & Co, kando ya Lebron James, Kylie Jenner, Donald Trump, na Charli D’Amelio.

Podcast ya ‘VIEWS’[hariri | hariri chanzo]

Kwenye Septemba 2018, Dobrik alitengeneza kituo cha tatu chake cha Youtube, Views Podcast. Alitumia kituo hicho kuonyesha video ya podcast zake. Dobrik alikuwa na mwonekano kwenye The Verge kama mmoja wa watengenzaji wa Youtube ameyegundua namna kufanikiwa kwenye kutengeneza podcasts kwa Youtube, hata kama kwanza, Youtube ni tovuni ya video.

Mada na mtindo wa vlog[hariri | hariri chanzo]

Kwenye habari ya Julai 2019, The Verge iliandikia vlog za Dobrik, ‘Vlog zake ni kama Friends, lakini kwa wawigizaji wa Youtube. Kwa msinigi, Dobrik alitengeneza vlog zinazofanana televisheni. Muziki, wahusika wa kawaida kusonga hadithi mbele, na kicheko kipo. Tunajua wakati wa kucheka kwa sababu Dobrik anacheka,”. Kwenye habari hio hio, mwandishi Julia Alexander alisema kwamba vlog za Dobrik zinafanana video za Vine na kwamba Dobrik aliwahamasisha wawigizaji wengine wengi.

Wahusika (“The Vlog Squad”)[hariri | hariri chanzo]

Vlog za Dobrik zinawahusisha rafiki zake ambao wanajuliwa kama “The Vlog Squad”. Kwa kawaida, watu wanaoshiriki kwenye kikundi hicho ni Jason Nash, Natalie Mariduena, Josh Peck, Zane Hijazi, Heath Hussar, Mariah Amato, Scotty Sire, Kristen McAtee, Nick Antonyan na ndugu zake Vardan na Suzy, Matt King, Toddy Smith, Corinna Kopf, Jeff Wittek, Joe Vulpis, Carly Incontro, na Erin Gilfoy. Wahusika wanao miwonekano chini ya wahusika wa kawaida ni Gabbie Hanna, Liza Koshy, Trisha Paytas, BigNik, Dom Zeglaitis, Seth Francois, Brandon Calvillo, Elton Castee, and Alex Ernst. Dobrik aliwasifa rafiki zake kwa kusema kwamba amefaulu kwa sababu ya rafiki zake.

Uhusiano kibiashara[hariri | hariri chanzo]

Dobrik ameshinda tuzo nyingi sana kwa uhusiano wake na kampuni kama SeatGeek, Chipotle, na Bumble. Imesemwa kwamba SeatGeek hasa ni kama mhusika wa vlog zake. Kampuni hizo zimemsaidia Dobrik kutengeneza video marufu sana, kama ‘Lid Flip Challenge’ na Chipotle na video za kuwanunulia rafiki za Dobrik magari.

Maisha binafsi[hariri | hariri chanzo]

Dobrik anao dada wawili na kaka mmoja, wanaoitwa Esther, Sarah, na Toby. Kama raia wa nchi nje ya USA aliyefika Marekani kama mtoto, Dobrik analindiwa kwa kufukuzwa nchini chini ya DACA (Deferred Action for Childhood Arrivals). Dobrik anaweza kuongea Kislovakia.

Dobrik alikuwa na uhusiano na mwigizaji wa Youtube anayeitwa Liza Koshy kutoka mwaka 2015 hadi mwaka 2018. Waliachana karibu na mwezi wa Juni 2018. Kwenye mwezi wa Mai 2019, Dobrik alimwoa Lorraine Nash, mama wa Jason Nash, kama utani kwa moja ya vlog zake. Waliachana baada ya mwezi mmoja.

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu David Dobrik kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.