Nenda kwa yaliyomo

David Bruck

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

David Isaac Bruck (amezaliwa Montreal, Quebec, Kanada, 1949) ni wakili wa utetezi wa jinai wa Kanada na Marekani, profesa wa sheria huko Washington na Lee University School of Law, na mkurugenzi wa Virginia Capital Case Clearinghouse.

Bruck alihudhuria Chuo Kikuu cha Harvard na Chuo Kikuu cha Sheria cha South Carolina.

Amewakilisha washtakiwa wenye hadhi ya juu, wakiwemo Ramzi bin al-Shibh, Dzhokhar Tsarnaev, Dylann Roof, na Susan Smith.

Maisha ya awali na elimu

[hariri | hariri chanzo]

Bruck alizaliwa na kukulia Montreal, Quebec, Canada.[1] Bruck ni mmoja wa watoto watatu wa Gerald, msimamizi wa nguo aliyestaafu, na Nina, mpiga picha.[1] Alisoma Chuo cha Harvard na alikuwa mchangiaji wa The Harvard Crimson.[2] Bruck alipata Shahada ya Sanaa magna cum laude kutoka Chuo Kikuu cha Harvard mnamo 1971.[3]

Baada ya chuo kikuu, Bruck alihudhuria Chuo Kikuu cha Sheria cha South Carolina. Alihudhuria shule ya sheria katika Chuo Kikuu cha South Carolina.[1] Wakati akiwa shule ya sheria, Bruck alifanya kazi kama mchomeleaji ilikuweza kulipia masomo yake kwasababu hakutaka kuwa na deni kwa familia yake baadae.[1] Alipokuwa katika Chuo Kikuu cha South Carolina, alikutana na rafiki yake na mwenzake, Judy Clarke. Alipata shahada yake ya J.D. katika mwaka wa 1975.

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 Cerio, Gregory. "Death on Trial" Ilihifadhiwa 3 Machi 2016 kwenye Wayback Machine.. people.com. People. Iliwekwa mnamo 16-09-2021
  2. "David I. Bruck | Writer Page | The Harvard Crimson". www.thecrimson.com. Iliwekwa mnamo 2021-09-16.
  3. "Meet Our Faculty". Washington and Lee University (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-09-16.