Nenda kwa yaliyomo

Dataz

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Dataz (alizaliwa Mbamba Bay, kando ya Ziwa Nyasa, mwaka 1984) ni rapa Mwanamke kutoka Tanzania.

Muda mfupi baada ya kuishi Mbamba Bay, alihama pamoja na wazazi wake kuelekea Morogoro. Alipofika Morogoro, alianza masomo yake ya awali. Kipaji chake cha kuimba kilianza kujulikana rasmi alipojiunga na shule ya sekondari ya Ifunda.[1].

Kazi ya Muziki

[hariri | hariri chanzo]

Dataz alianza kuimba na kurap akiwa na rapa mwenzake wa kike aitwae Bad G, ambapo walishirikiana kwa pamoja kwenye muziki kwa kipindi kifupi, mpaka sasa kila mmoja anaimba pekeyake.

Dataz nyimbo yake ya kwanza iliitwa “Kitimtim” ambapo ilichukuwa nafasi kubwa kwenye vyombo vya habari nchini Tanzania.

Aina ya rap iliyo na nakala zinazo elezea msingi wa kutiisha wanawake. Wakati hip hop ya Marekani imejaa kumbukumbu za kutiisha wanawake, Rap ya Kiswahili haina lugha kama hiyo inayotumika kwa wanawake. Kwa sababu dini imecheza sehemu kubwa katika maisha ya wasanii wanao rap, wanakuja kwenye njia panda pale wanapotaka kuigia rap ya kigansta inayotiisha wanawake. Hii inaacha nafasi ya ukweli kwa wasanii ambayo pia ni muhimu kwenye rap ya Kiswahili kama kwenye rap ya kimarekani,lakini pia inaacha nafasi kubwa ya mandhari ya hip hop ya wanawake kuingia. [2]

Dataz alilaumu sana uwepo wa marapa wachache wakike nchini Tanzania ambapo marapa wakike ambao walikuwa na nafasi kubwa katika jamii ikiwemo rapa MCing naDJing walijihusisha zaidi na uhuni pamoja na matumizi ya mabavu, mfano kuiga gangsta rap ya Marekani.

Msanii mwenzake wa rap Tuni wa Nubian Motown alisema“wasichana wengi wanaona aibu kujihusisha na rap kwasababu ya mtazamo kwamba rap ni vitu vya kuime na inahusiana na magenge,vurugu na tabia zote za kishetani.”Kitu ambacho kinakosekana kwenye rap ya Kiswahili,lakini ni kikubwa kwenye ushawishi wa rap ya kimarekani[3]

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-11-29. Iliwekwa mnamo 2021-03-06.
  2. Hip Hop Culture And The Children Of Arusha: ‘Ni wapi Tunakwenda’ Sidney J. Lemelle
  3. Africanhiphop.com :: African Rap :: 10 years online

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Dataz kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.