Cynthia Wandia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Cynthia Wandia ni Mhandisi wa umeme nchini Kenya, Mjasiriamali, Mwanamke Mfanyabiashara na Meneja wa Kampuni, ambaye ni Mkurugenzi mkuu na mwanzilishi wa Kwara Limited, jukwaa la benki ya mtandaoni na simu za mkononi la Kenya katika mfumo wa ushirikiano wa kifedha, vyama vya mikopo na benki za jamii.[1] Wakati huo huo anafanya kazi kama Mkurugenzi Mkuu wa ASTRA Innovations, kampuni ya biashara iliyopo nchini Ujerumani ambaye ni mwanzilishi.[2][3]

Maisha ya Nyuma na Elimu[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa nchini Kenya, mwaka 1986.[2] Alisoma Shule ya wasichana Alliance katika mji wa Kikuyu, Wilaya ya Kiambu, nchini Kenya. Kisha alienda Marekani na kujiunga na Chuo Kikuu cha Yale mwaka 2005. Cynthia alihitimu mwaka 2009 nakupata Shahada ya Sayansi katika Uhandisi wa Umeme. Alifuatilia masomo hayo katika ngazi ya juu ya Usimamizi katika Chuo cha Dartmouth.[4]

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Cynthia alitumia miezi 6 katika mwaka 2010 huko Monterrey, Meksiko, akifanya kazi kama mshauri wa maendeleo ya biashara wa Aceleradora de Empresas ITESM. Baadae alihamia Düsseldorf, Ujerumani na kufanya kazi na E.ON, katika kitengo chao cha kimataifa cha bidhaa, kama sehemu ya mpango wa kufuzu kwa biashara. Baadhi ya mafunzo yalifanyika katika mji wa Madrid, Hispania. Alifanya kazi katika nafasi hiyo kwa muda wa mwaka mmoja na nusu, hadi Mei 2012.[4]

Kwa kipindi cha miaka miwili na miezi 6, alifanya kazi katika kampuni ya E.ON, katika mji wa Essen, Ujerumani, kama Mtaalamu wa Utendaji wa Meli kwa takriban nusu ya kipindi hicho, kisha kama Meneja wa Miradi Maalum. Mnamo Desemba 2014, aliondoka E.ON na kuanzisha Astra Innovations.[4]

Astra Innovations, ni chanzo cha mitambo ya kuzalisha umeme wa gesi na umeme wa maji, hununua mitambo hiyo kwa bei nafuu na kuziuza kwa wazalishaji wa umeme wa Kusini mwa Jangwa la Sahara, Asia ya Kusini na Amerika Kusini.[3]

Vigezo vingine[hariri | hariri chanzo]

Cynthia Wandia anaripotiwa kujua lugha ya Kiingereza, Kihispania, Kifaransa, Kijerumani na Mandarin.[2] Mnamo mwaka 2018, gazeti la Business Daily Africa na gazeti la Kiingereza la kila siku nchini Kenya, yaliripoti kuwa Cynthia Wandia, ni mmojawapo wa Kenya Top 40 Under 40 Women.[2]

Kampuni yake ya hivi karibuni, ambayo alianzisha na anayofanya kazi kama Mkurugenzi Mkuu, ni Kwara Limited, programu ya benki ya mtandaoni na ya simu ya mkononi ambayo husaidia vyama vya ushirika, benki za jamii na vyama vya mikopo kutunza mahitaji ya kifedha na nafasi za wanachama wao kwa wakati halisi. Hii inaruhusu taasisi kujibu kwa haraka mahitaji ya wanachama wao, na hivyo kudumisha idadi kubwa ya wateja wenye furaha, kuendeleza faida katika mchakato huo.[1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 Mariama Boumanjal (11 December 2019). "Meet Kwara, a startup in the new Africa Immersion program". Google Inc. Iliwekwa mnamo 16 February 2020.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 Business Daily Staff (September 2018). "Top 40 Under 40 Women In Kenya 2018". Business Daily Africa. Nairobi. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-09-29. Iliwekwa mnamo 6 October 2018.  More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  3. 3.0 3.1 Wharton Business School (13 April 2016). "Power Shift: An Innovative Solution for the African Energy Market". Philadelphia: Wharton School of Business. Iliwekwa mnamo 6 October 2018.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  4. 4.0 4.1 4.2 Cynthia Wandia (6 October 2018). "Cynthia Wandia: Co-founder & Managing Director of Astra Innovations". Linkedin.com. Iliwekwa mnamo 6 October 2018.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)