Nenda kwa yaliyomo

Cristina Sánchez

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Cristina Sánchez akiwa kwenye uwanja wa mapigano.

Cristina Sánchez de Pablos (alizaliwa 20 Februari 1972) ni Mhispania mpiganaji wa ng'ombe ambaye alipata umaarufu miaka ya 1990 kwa kuwa mmoja wa wapiganaji wa ng’ombe wa kwanza mwanamke.[1] Alikuwa mwanamke wa kwanza kumaliza alternativa yake ndani ya Ulaya.[1]

Cristina Sánchez de Pablos alikuwa mpiganaji wa ng'ombe mtaalamu katika ulingo wa ng'ombe ndani ya Ekuador na Meksiko na hufanya maonyesho mengi ndani ya Hispania.[1] Kwa mara ya kwanza alionekana kama mpiganaji wa ng’ombe ndani ya Madrid 13 Februari 1993. Wakati wa kazi yake Sanchez, alikata jumla ya masikio 316 ya ng’ombe. Alistaafu mwaka 1999 na kuolewa na Mreno Alexandre da Silva mwaka 2000.

Sanchez alichukuliwa na wengi kuwa mwakilishi wa harakati za jinsia ya kike za miaka ya 1990, kwa kuwa mchezo wa ng'ombe ulitawaliwa na wanaume.[2] Alikuwa pia mada ya kipindi cha habari cha Univision TV Primer Impacto, ambapo Maria Celeste Arraras aliwasilisha makala inayomhusu.

Tazama Pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. 1.0 1.1 1.2 Orlean, Susan. "The Woman Who Fought Bulls". The Stacks (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-04-04. Iliwekwa mnamo 2020-06-29.
  2. Madrid, Guy Hedgecoe in. "Male-dominated domain of bullfighting engulfed in gender controversy". The Irish Times (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-06-29.

Kujisomea

[hariri | hariri chanzo]
  • "Cristina Sánchez (bullfigher)", in Outstanding Women Athletes: Who They Are and How They Influenced Sports in America by Janet Woolum (Phoenix: Oryx Press, 1998), pp. 214–215

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Cristina Sánchez kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.