Comme Un...

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Comme Un...
Comme Un... Cover
Studio album ya Jean Baron
Imetolewa 1991
Imerekodiwa 1990-1991
Aina Soukous
Lebo Jimmy's Production
Mtayarishaji Jimmy Houetinou


"Comme Un..." ni jina la albamu ya kwanza iliyotoka mwaka 1991 kutoka kwa msanii wa muziki wa soukous kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jean Baron. Albamu hii ni moja kati ya albamu bora kabisa za Baron na albamu pekee kutoka kwa msanii huyu hadi umauti ulipomkuta. Nyimbo kali kutoka katika albamu hii ni pamoja na Mami Lolo, Koudia Ndambou, Comme Un ... na Pantalon Moriba. Huu ulikuwa utaratibu wa kawaida kwa kundi la Loketo kila msanii wake kurekodi albamu ya kujitegemea na kuungwa mkono kamilifu kutoka kwa wanachama wenzake. Alianza Aurlus Mabelle kisha Diblo Dibala, Baron halafu wengineo.

Orodha ya nyimbo[hariri | hariri chanzo]

Zifuatazo ni orodha kamili ya nyimbo zinapatikana katika albamu hii.

  • 1- Mami Lolo
  • 2 - Nabeleli
  • 3 - Koudia Ndambou
  • 4 - Pantalon Moriba
  • 5 - Comme Un ...
  • 6 - Lutter Lutter

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]