Chura-sugu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Chura-sugu
Chura-sugu wa Garman
Chura-sugu wa Garman
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Amphibia (Wanyama wanaoanza maisha kwenye maji na kuendelea nchi kavu)
Nusungeli: Lissamphibia (Amfibia waliopo bado)
Oda: Anura (Vyura)
Nusuoda: Neobatrachia
Familia: Bufonidae
Gray, 1825
Ngazi za chini

Jenasi 6 katika Afrika:

Vyura-sugu ni aina za vyura wa familia Bufonidae katika oda Anura ambao ngozi yao ina sugu. Wana jozi ya tezi kichogoni zinazochoza sumu ya neva (bufotoxin) ili kuzuia maadui.

Vyura hawa huishi kwa nchi kavu au juu ya miti lakini takriban spishi zote hutaga mayai katika maji. Mayai hayo hutoa ndubwi. Spishi za jenasi Nectophrynoides (vyura-sugu msitu) hazitagi mayai lakini huzaa vyura wadogo, kwa sababu ndubwi wanatoka kwa mayai ndani ya kirijaova cha jike na kukua mpaka vyura.

Spishi za Afrika ya Mashariki[hariri | hariri chanzo]

Spishi za pande nyingine za Afrika[hariri | hariri chanzo]


Picha[hariri | hariri chanzo]