Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Ruaha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Chuo Kikuu cha Kikatoliki Ruaha ni chuo kikuu cha Kanisa Katoliki[1] kinachopatikana Iringa, Tanzania[2].

Chuo kilianzishwa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania kikasajiliwa kama chuo kikuu kishiriki cha Ruaha kikiwa chini ya Chuo Kikuu cha St. Augustine cha Tanzania.

Chuo kinaongozwa kwa misingi ya kanuni za Kanisa juu ya elimu ya juu. Hata hivyo, chuo kinajitegemea katika utawala wake na utoaji wa elimu na kinapokea wanafunzi wa imani zote bila ya ubaguzi.

Taaluma[hariri | hariri chanzo]

Chuo kina vitivo vifuatavyo:

  • Kitivo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
  • Kitivo cha Sheria
  • Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Jamii
  • Kitivo cha Afya ya Jamii
  • Kurugenzi ya Mafunzo ya muda mfupi na Elimu ya Kujiendeleza

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Chuo Kikuu cha Ruaha. www.rucu.ac.tz. Jalada kutoka ya awali juu ya 2019-11-07. Iliwekwa mnamo 2019-11-07.
  2. Wayback Machine. web.archive.org (2015-09-24). Jalada kutoka ya awali juu ya 2015-09-24. Iliwekwa mnamo 2021-06-19.
  1. "Register of Universities" (PDF). Tanzania Commission for Universities. Archived from the original (PDF) on 24 September 2015. Retrieved 15 July 2013.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Kigezo:Vyuo vikuu vya Tanzania

Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Ruaha kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.