Shoronjano
Mandhari
(Elekezwa kutoka Chloropeta)
Shoronjano | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Jenasi 3, spishi 8 za shoronjano:
|
Shoronjano ni ndege wadogo wa jenasi Arundinax, Calamonastides na Iduna katika familia Acrocephalidae. Spishi nyingine za familia hii zinaitwa shoro kwa ufupi. Ndege hawa wana rangi ya kahawa mgongoni na njano chini. Wanatokea misitu au mabwawa ya mafunjo (Shoronjano domo-jembamba) ya Afrika. Hula wadudu. Hujenga tago lao kwa umbo wa kikombe au kikapu kwa majani na pengine vijiti. Tago la kibwirosagi domo-jembamba limefungika mabua ya mafunjo. Jike huyataga mayai 2-6.
Spishi za Afrika
[hariri | hariri chanzo]- Calamonastides gracilirostris, Shoronjano Domo-jembamba (Papyrus Flycatcher-warbler)
- Iduna natalensis, Shoronjano Utosi-mweusi (Yellow Flycatcher-warbler)
- Iduna opaca, Shoronjano Zeituni Magharibi (Western Olivaceous Warbler)
- Iduna pallida, Shoronjano Zeituni Mashariki (Eastern Olivaceous Warbler)
- Iduna similis, Shoronjano-milima (Mountain Flycatcher-warbler)
Spishi za Eurasia
[hariri | hariri chanzo]- Arundinax aedon (Thick-billed Warbler)
- Iduna caligata (Booted Warbler)
- Iduna rama (Sykes's Warbler)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Shoronjano zeituni magharibi
-
Shoronjano zeituni mashariki
-
Shoro wa Lantz
-
Shoro wa Madagaska
-
Thick-billed warbler
-
Booted warbler
-
Sykes's warbler