Nenda kwa yaliyomo

Charles Pedersen

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Charles John Pedersen (3 Oktoba 190426 Oktoba 1989) alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Marekani akiwa amezaliwa nchini Korea na kulelewa nchini Japani. Babake alikuwa Mnorwei na mamake Mjapani. Jina lake la Kijapani lilikuwa Yoshio. Mwaka wa 1922 alihamia nchini Marekani. Hasa alichunguza usanisi wa etha maalumu. Mwaka wa 1987, pamoja na Donald Cram na Jean-Marie Lehn alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia.


Makala hii kuhusu mshindi wa Tuzo ya Nobel bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Charles Pedersen kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.