Carole Nyakudya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
carole nyakudya
Nchi zimbabwe
Kazi yake mwanamuziki wa injili

Carole Nyakudya ni Mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili wa nchini Zimbabwe, Mjasiriamali,[1][2] mwanachama mwanzilishi wa kwaya ya Zimpraise na ni mtangazaji wa televisheni maarufu ya mtandaoni, Zimbolive TV.

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa Zimbabwe 1978,Nyakudya alikulia kwenye jiji la Bulawayo,kisha 1997 alihamia uingereza kama mtaalamu wa afya ya akili NHS.[3] Nyakudya ana stashahada ya afya ya akili ambayo aliipata chuo kikuu cha Birmingham. Shahada ya mafunzo ya afya katika chuo kikuu cha Wolverhampton na Shahada ya Uzamili ya afya ya umma na maendeleo aliyosomea chuo kikuu cha Birmingham

Carole Nyakudya alijulikana zaidi mwaka 2005 alipotoa albamu ya kwanza hii ni sasa ambayo iliteuliwa kama albamu bora ya mwaka katika tuzo za kitaifa mwaka 2005. Nyakundya ni mwanachama mwanzilishi wa kikundi cha nyimbo za injili cha Zimpraise kwaya kilichoanzishwa 2006.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Carole Nyakudya mixes gospel and mental health awareness – The Sunday News". www.sundaynews.co.zw. Iliwekwa mnamo 2023-02-26. 
  2. "Gospel-inspired fun day". www.thezimbabwean.co. Iliwekwa mnamo 2023-02-26. 
  3. The Chronicle. "Covid-19 amplifies gap in Africa’s mental healthcare services". The Chronicle (kwa en-GB). Iliwekwa mnamo 2023-02-26. 
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Carole Nyakudya kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.