Carola Kinasha
Carola Daniel Amri Kinasha (alizaliwa Longido, Mkoa wa Arusha, Tanzania, mnamo Machi mwaka 1962) ni mwanamuziki wa kike wa kitanzania.
Baada ya kumaliza masomo ya elimu ya msingi huko Longido, alihamia jijini Dar Es Salaam ambapo alipata elimu ya sekondari na ya chuo kikuu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Carola amekuwa akijihusisha na masuala ya muziki tangu mwaka wa 1988.
Ameshiriki katika miradi na matamasha mbalimbali ya kimuziki, ndani na nje ya Tanzania. Pia amekuwa mtetezi wa haki za binadamu kwa ujumla akiweka msisitizo zaidi kwenye haki za wasanii wa Tanzania. Anaamini kuwa ili tasnia ya sanaa ya Tanzania iweze kukua na kujulikana kimataifa ni muhimu kurejesha elimu ya sanaa kwenye shule zetu. Pia kuwa na sehemu za kufanyia shughuli za sanaa kwenye kila kitongoji. [1]
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Tovuti ya Women's Voice Ilihifadhiwa 5 Februari 2005 kwenye Wayback Machine.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Carola Kinasha kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |