Nenda kwa yaliyomo

Brook Benton

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Brook Benton

Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Benjamin Franklin Peay
Amezaliwa (1931-09-19)Septemba 19, 1931
Lugoff, South Carolina, U.S.
Amekufa Aprili 9, 1988 (umri 56)
Queens, New York, U.S.
Aina ya muziki Pop, R&B, soul
Kazi yake Singer, songwriter, actor
Ala Vocals
Miaka ya kazi 1958–1988
Studio Mercury, Cotillion, RCA


Brook Benton (19 Septemba 1931 – 9 Aprili 1988) alikuwa mwimbaji na mtunzi wa nyimbo wa Marekani ambaye alijulikana katika mienendo ya rock and roll, R$B, na pop mwishoni mwa miaka ya 1950 na mwanzoni mwa miaka ya 1960 ambapo alipokea umaarufu kwa nyimbo kama "It's Just A Matter Of Time" na "Endlessly", nyingi zao ambazo alishiriki kuandika. Alirejea mnamo 1970 na wimbo taratibu wa "Rainy Night in Georgia." Benton alishinda zaidi ya vibao katika chati ya Billboard kama msanii na pia akaandika vibao vilivyovuma kwa wasanii wengine.

Kuingia katika Umaarufu

[hariri | hariri chanzo]

Benjamin Franklin Peay alizaliwa mnamo 19 Septemba 1931 kule Lugoff. Alipokuwa mchanga, Peay alijifurahisha kuimba nyimbo za kiinjili na alikuwa akiandika nyimbo. Mnamo 1948 alienda to New York kusomea muziki. Alijiunga na kutoka katika makundi mengi ya muziki wa Gospel kama vile The Langfordaires, The Jerusalem Stars, na The Golden Gate Quartet. Aliporejea katika jimbo lake la nyumbani, alijiunga na kundi la R$B, ‘’The Sandmen’’ na akarejea New York kupata umaarufu makubwa na kundi lake. Kundi hili halikuwa na mafanikio makubwa na lebo yao Okeh Records, iliamua kumchochea Peay kuwa mwimbaji wa solo, huku akibadilisha jina lake kuwa ‘’’Brook Benton’’’ kwa ushawishi wa mkuu wa lebo hiyo Marv Halsman.[1].

Brook aliishivyema akiwatungia nyimbo wasanii kama as Nat King Cole, Clyde McPhatter (aliyemtungia wimbo uliovuma "A Lover's Question"), na Roy Hamilton na akishiriki kama mtayarishi msaidizi. Punde alitoa albamu yake ya kwanza "A Million Miles from Nowhere" ambayo iliongoza katika chati. Hatimaye alihamia lebo ya Mercury ambayo baadaye ilikuja kumletea ufanisi mkubwa.

Ufanisi Mkuu

[hariri | hariri chanzo]

Hatimaye 1959 aliingia umaarufuni na vibao vyake vilivyovuma vya It's Just a Matter of Time" na "Endlessly". "It's Just a Matter of Time" ilifikia kileleni katika nafasi ya 3 katika chati za U.S. Billboard Hot 100 wakati "Endlessly" ikifika #12. nyimbo hizi zote zilitungwa naye kwa ushirikiano na Clyde Otis. Mwanzoni zilikuwa zimekabidhiwa kwa Nat King Cole lakini Otis alipokuwa afisa wa A$R katika ‘’Mercury’’ alimshawishi Benton kutia mkataba na lebo hiyo na azitayarishe mwenyewe huku akimwomba Cole asizitayarishe ilivyokuwa imepangwa. .[2]. Benton aliufuata ufanisi huu kwa mshururu wa vibao vilivyovuma vikiwemo "So Many Ways" (#6), "Hotel Happiness" (#3), "Think Twice" (#11), "Kiddio" (#7), na "The Boll Weevil Song" (#2). Mnamo 1960 aliibuka na hit mbili kwa Top 40 katika kumi bora zaidi, ambazo zilikuwa za ushirikian wa ‘’duet’’ na Dinah Washington: "Baby (You've Got What It Takes)" (#5) na pia "A Rockin' Good Way (To Mess Around and Fall in Love)" (#7).[3].

Pia alitayarisha toleo lake la "Take Good Care of Her" mnamo 1962. Mnamo kati na mwishoni mwa 1960s, Benton alitayarisha kwa lebo za RCA Records na Reprise Records akiwa na mafanikio machache. Hatimaye 1969 alitia mkataba kandarasi na Cotillion Records, shirika dogo la Atlantic Records, ambapo mwaka uliofuatia alikuwa na hit yake kuu ya mwisho, "Rainy Night in Georgia"[3].

Hatimaye Benton alikuwa na single 49 kwa Billboard Hot 100, hi=uku nyimbo zingine zikiorodheshwa katika chati za Billboard za rhythm and blues, easy listening, na Christmas music[4]

Albamu ya mwisho aliyoitengeneza ilikuwa Fools Rush In, ambayo ilitoka baadaye mnamo 2005. Kwa wakati mmoja alikuwa akifanya kazi na lebo ya Groove Records.[5].

Brook aliaga dunia kutokana na shida katika uti wa mgongo (menengitis) katika mji wa Queens, New York katika umri wa 56 mnamo 9 Aprili 1988.

Diskografia

[hariri | hariri chanzo]
Mwaka Albamu U.S. Pop
1959 This Time of Year 12
1961 Golden Hits 82
1961 The Boll Weevil Song And 11 Other Great Hits 70
1962 If You Believe 77
1962 Singing the Blues - Lie to Me 40
1963 Golden Hits, toleo la 2 82
1967 Laura (What's He Got That I Ain't Got) 156
1969 Do Your Own Thing 189
1970 Brook Benton Today 27
1970 Homestyle 199
1977 The Incomparable Brook Benton - 20 Greatest Hits (Warwick) -
Mwaka Single US Pop US R&B US AC UK Singles Chart[6] Album
1958 "A Million Miles from Nowhere" 82 - - - -
1959 "Endlessly" 12 3 - 28 -
1959 "Hurtin' Inside" 78 23 - - -
1959 "This Time of the Year" - - - - This Time of the Year
1959 "It's Just a Matter of Time" 3 1 - - It's Just a Matter of Time
1959 "So Close" 38 5 - - -
1959 "So Many Ways" 6 1 - - -
1959 "Thank You Pretty Baby" 16 1 - - -
1959 "With All My Heart" 82 - - - -
1960 "Baby (You've Got What It Takes)" (akimshirikisha Dinah Washington) 5 1 - - -
1960 "Fools Rush In (Where Angels Fear to Tread)" 24 5 - 50 Songs I Love to Sing
1960 "Someday You'll Want Me to Want You" 93 - - - -
1960 "Kiddio" 7 1 - 41 -
1960 "A Rockin' Good Way" (na Dinah Washington) 7 1 - - -
1960 "The Same One" 16 21 - - -
1960 "The Ties That Bind" 37 15 - - -
1961 "For My Baby" 28 2 - - -
1961 "Frankie and Johnny" 20 14 6 - The Boll Weevil Song
1961 "It's Just a House Without You" 45 - 8 - -
1961 "Think Twice" 11 6 - - -
1961 "The Boll Weevil Song" 2 2 1 30 The Boll Weevil Song
1962 "Hit Record" 45 19 - - -
1962 "Lie to Me" 13 3 - - Singing The Blues
1962 "Revenge" 15 12 - - -
1962 "Shadrack" 19 - - - -
1962 "The Lost Penny" 77 - - - -
1962 "Still Waters Run Deep" 89 - - - -
1962 "Walk on the Wild Side" 43 - - - -
1963 "Hotel Happiness" 3 2 - - -
1963 "I Got What I Wanted" 28 4 14 - Singing The Blues
1963 "Dearer Than Life" 59 - - - -
1963 "My True Confession" 22 7 8 - Singing The Blues
1963 "Two Tickets to Paradise" 32 15 8 - -
1964 "Another Cup of Coffee" 47 47 13 - -
1964 "Going Going Gone" 35 35 - - -
1964 "A House is Not a Home" 75 75 13 - -
1964 "Too Late to Turn Back Now" 43 43 14 - -
1964 "Lumberjack" 53 53 15 - -
1964 "Do It Right" 67 67 - - -
1965 "Love Me Now" 100 - 37 - -
1965 "Mother Nature, Father Time" 53 26 9 - Mother Nature, Father Time
1967 "Laura (What's He Got That I Ain't Got)" 78 - 37 - -
1968 "Weakness in a Man" - - 36 - -
1968 "Do Your Own Thing" 99 - 26 - -
1969 "Nothing Can Take the Place of You" 74 11 - - -
1970 "Don't It Make You Want to Go Home" 45 31 4 - Home Style
1970 "My Way" 72 25 35 - Today
1970 "Rainy Night in Georgia" 4 1 2 - Today
1971 "Shoes" 67 18 18 - -
1978 "Making Love is Good for You" - 49 - - -
  1. ""Marv Goldberg, Marv Goldberg's R&B Notebooks: The Sandmen"". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-03-30. Iliwekwa mnamo 2010-01-21.
  2. Colin Escott, "Clyde Otis: Looking Back". Goldmine, 1 Oktoba 1993, pp. 42-43.
  3. 3.0 3.1 Brook Benton at Allmusic
  4. Joel Whitburn, Top Pop Singles 1955-1999 (Menomonee Falls, WI: Record Research, 2000), 48-49.
  5. Shaw, Arnold (1978). Honkers and Shouters. New York: Macmillan Publishing Company. ku. 463. ISBN 0-02-061740-2.
  6. Roberts, David (2006). British Hit Singles & Albums (tol. la 19th). London: Guinness World Records Limited. uk. 54. ISBN 1-904994-10-5.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]