It's Just a Matter of Time

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

"It's Just a Matter of Time" ni wimbo wa ‘’pop’’ ulioandikwa na Brook Benton kwa ushirikiano wa Clyde Otis. Toleo la asili lililorekodiwa na Benton liliongoza katika chati za the Billboard rhythm & blues mnamo 1959 na kufikia kilele katika nafasi ya 3 katika chati za the ‘’Billboard Hot 100 pop’’, wa kwanza katika mshururu wa nyimbo za Benton zilizovuma mnamo miaka ya 1970[1].

Wimbo huu hatimaye ulipata mwelekeo mpya kama mwenendo wa country huku matoleo yake makuu yakitayarishwa na wasanii watatu mashughuli wa country katika miaka ya 1970s na 1980s. Mawii kati ya matolao haya yalivuma katika nafasi ya kwanza. [2]

Kiini na Mafanikio ya mwanzo[hariri | hariri chanzo]

“It's Just a Matter of Time”
Single ya Brook Benton
Imetolewa 1958
Urefu 2:28
Mtunzi Brook Benton, Belford Hendricks, Clyde Otis
Certification Gold

Utunzi[hariri | hariri chanzo]

Brook Benton na Clyde Otis walianza kama timu ya utunzi wa nyimbo katika miaka ya baadaye ya 1950, huku wakitunga vibao kama "Looking Back" ya Nat King Cole na "A Lover's Question" ya Clyde McPhatter. Wakati wa vikao vya kuandika nyimbo, Benton alionyesha kutatizika kwa nini hawakuwa wanaangukia mawazo bora na Otis akajibu, "It's just a matter of time, Brook" (Jipe muda tu Brook). Maeno hayo yaliwachochea kuandika wimbo wa kimapenzi kutoka kwa mtazamo wa mwanaume anayemkosa sana mpenziwe lakini anaamini atamrudia. [3]

Nafasi katika Chati[hariri | hariri chanzo]

Chati (1959) Kilele
U.S. Billboard Hot 100 3
U.S. R&B Singles 1
Alitanguliwa na
"Stagger Lee"
wa Lloyd Price
Billboard Hot R&B Singles Singe ya kwanza
9 Machi-10 Mei 1959
Akafuatiwa na
"Kansas City"
ya Wilbert Harrison

Matoleo ya Country[hariri | hariri chanzo]

Toleo la Sonny James[hariri | hariri chanzo]

“It's Just a Matter of Time”
Single ya Sonny James
Imetolewa Januari 1970
Urefu 2:35
Mtunzi Brook Benton, Belford Hendricks, Clyde Otis

Toleo la kwanza la Cover lililotayarishwa na Sonny James; lilivuma katika mienendo ya Country na kukaa kileleni mwa chati za Billboard magazine Hot Country Singles kwa wiki nne mnamo Februari 1970. Huu ulikuwa wimbo wa kumi wa Jaames katik mshururu wa nyimbo zake 16 zilizoongoza katika chati hizo kati ya 1967-1971. James aliuimba wimbo huu katika tamasha za The Ed Sullivan Show mnamo 11 Januari 1970 (Siku chache baada ya Single kutayarishwa) na Hee Haw mnamo 21 Januari[4]

Nafasi katika Chati[hariri | hariri chanzo]

Chati (1970) Kilele
U.S. Billboard Hot Country Singles 1
U.S. Billboard Hot 100 87
Alitanguliwa na
"A Week in a Country Jail" ya Tom T. Hall
Billboard Hot Country Singles
Single Bora zaidi

14 Februari-7 Machi 1970
Akafuatiwa na
"The Fightin' Side of Me" ya Merle Haggard

Toleo la Glen Campbell[hariri | hariri chanzo]

“It's Just a Matter of Time”
Single ya Glen Campbell
A-side It's Just a Matter of Time
B-side Gene Autry, My Hero
Imetolewa Oktoba 1985
Urefu 2:27
Mtunzi Brook Benton, Belford Hendricks, Clyde Otis

Mnamo 1985, Glen Campell aliutayarisha wimbo huu na kuutoa kama single. Toleo lake lilipanda kufikia nafasi ya saba katika chati za Billboard Hot Country Singles mnamo Februari 1986.

Nafasi katika Chati[hariri | hariri chanzo]

Chati (1985) Kilele
U.S. Billboard Hot Country Singles 7
Canadian RPM Country Tracks 7Toleo la Randy Travis[hariri | hariri chanzo]

“It's Just a Matter of Time”
“It's Just a Matter of Time” cover
Single ya Randy Travis
B-side "This Day Was Made for You and Me"
Urefu 3:56
Mtunzi Brook Benton, Belford Hendricks, Clyde Otis


Randy Travis alikuwa msanii wa tatu kufanikuiwa na wimbo huu. Aliutoa mnamo Agosti 1989 ukiongoza albamu ya Single No Holdin' Back. Toleo la Travis lilikuwa wimbo wake wa kumi kufika #1 katika chati za Billboard Hot Country Singles.

Rendition yake Travis ilitayarishwa awali katika albamu ya Rock, Rhythm & Blues, iliyoshirikisha mkusanyiko wa vibao kumi vikiwemo vibao kutoka miaka ya vilivyovuma miaka ya 1950 ambavyo vimefanya na wasanii wa miaka ya 1980. Baadaye wimbo huu ulishirikishwa katika albamu ya No Holdin' Back baada ya Travis na wengine walipendezwa na utayarishi wao[5].

Nafasi Katika Chati[hariri | hariri chanzo]

Chati (1989) Kilele
U.S. Billboard Hot Country Singles 1
Canadian RPM Country Tracks 1
Alitanguliwa na
"Yellow Roses"
yake Dolly Parton
Billboard Hot Country Singles
Single ya Kwanza

2 Desemba 1989
Akafuatiwa na
"If Tomorrow Never Comes"
yake Garth Brooks
Alitanguliwa na
"Bayou Boys"
yake Eddy Raven
RPM Country Tracks
Single bora zaidi yake Randy Travis

2 Desemba-9 Desemba 1989
Akafuatiwa na
"Yellow Roses"
yake Dolly Parton

Virejeleo na Viini[hariri | hariri chanzo]

Virejeleo[hariri | hariri chanzo]

  1. Allmusic — "It's Just a Matter of Time"
  2. Roland, Tom, "The Billboard Book of Number One Country Hits," Billboard Books, Watson-Guptill Publications, New York, 1991 (ISBN 0-8230-7553-2), p. 35
  3. Colin Escott, "Clyde Otis: Looking Back". Goldmine, 1 Oktoba 1993, pp. 42-43.
  4. ibid.
  5. Roland, p. 570.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]