Nenda kwa yaliyomo

Brigitte Bardot

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Brigitte Bardot

Brigitte Bardot, 1962
Amezaliwa 28 Septemba 1934
Ufaransa
Amekufa 28 Desemba 2025
Kazi yake mwigizaji wa filamu, mwanamitindo, mwimbaji na mwanaharakati wa haki za wanyama
Brigitte Bardot, 1968.

Brigitte Bardot (28 Septemba 1934 - 28 Desemba 2025) alikuwa mwigizaji wa filamu, mwanamitindo, mwimbaji na mwanaharakati wa haki za wanyama wa Ufaransa. Ni miongoni mwa waigizaji-waimbaji waliokuwa na wapenzi zaidi katika miaka ya 1950 na 1960. Ni mmoja kati waigizaji wachache wa kutoka Ulaya ambao vyombo vya habari vya Marekani vimempa heshima kubwa: yeye alibahatika kuwa na sifa kubwa kabisa katika Amerika.

Kunako miaka ya 1970 hivi, baada ya kustaafu shughuli zake za utoaji wa burudani, Bardot akaamua kuwa mwanaharakati wa haki za wanyama, ambayo shughuli hiyo mpaka kifo chake aliiendeleza.

Kunako miaka ya 1990 alizungumza mengi kuhusiana na mtazamo wake wa kisiasa juu ya masuala ya uhamiaji, Uislamu kuingia nchini Ufaransa na masuala ya kujamiiana waume kwa waume, yaani, mashoga-wasenge. Aliponda sana vitu hivyo hata kuchukiwa na watu waliopo katika jamii hizo.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Brigitte Bardot kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.