Nenda kwa yaliyomo

Brangelina

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitt na Jolie kwenye sherehe ya 81st Academy Awards mnamo Februari 2009

Brangelina ni jina linalojumuisha muigizaji Brad Pitt wa kutoka Marekani aliyeigiza katika filamu zaidi ya 40 (kama Fight Club, Se7en, Mr. & Mrs. Smith) na Angelina Jolie ambaye ni balozi wa shirika la Umoja wa Mataifa na vilevile muigizaji wa filamu kama Lara Croft: Tomb Raider na Changeling.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Brad Pitt

[hariri | hariri chanzo]

Katika miaka ya nyuma, Pitt amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na waigizaji wengi kama Robin Givens, Jill Schoelen, na Juliette Lewis.[1] Pitt pia alikuwa mchumba wake Gwyneth Paltrow, aliyekuwa na uhusiano naye kuanzia mwaka wa 1995 hadi 1997.[2]

Pitt alionana na muigizaji wa kipindi cha Friends aitwaye Jennifer Aniston mnamo 1998 na wakaoana mjini Malibu mnamo 29 Julai 2000.[3] Mnamo Januari 2005, Pitt na Aniston walitangaza kuwa wameachana baada ya kuoana kwa muda ya miaka saba.

Angelina Jolie

[hariri | hariri chanzo]
Makala kuu: Angelina Jolie

Mnamo 28 Machi 1996, Jolie aliolewa na muigizaji Muingereza Jonny Lee Miller.[4] Jolie na Miller waliachana mwaka uliofuata na talaka ikatolewa mnamo 3 Februari 1999. Mnamo 5 Mei 2000, aliolewa na muigizaji wa Marekani anayeitwa Billy Bob Thornton, na wakawachana mnamo 27 Mei 2003.

Uhusiano wao

[hariri | hariri chanzo]

Jolie na Pitt walikutana walipokuwa wanaigiza katika filamu ya Mr. & Mrs. Smith na uhusiano wao ulijulikana sana kwenye Hollywood .[5]. Inasemekana kuwa Pitt na Jolie walipendana pindi Pitt bado alikuwa na Jennifer Aniston, lakini wote wamekataa madai haya; wakisema kuwa walipendana walipukuwa wakiigiza filamu hii.[6] Uhusiano wa Pitt na Jolie ulithibitishwa wakati picha zilitoka za kuonyesha Pitt akiwa na Jolie na mwanawe Maddox kwenye bahari nchini Kenya.[7] Wawili hawa walionekana wakiwa pamoja mara nyingi, na watangazaji wakawabandika wapenzi hawa jina la "Brangelina".[8] Mnamo 11 Januari 2006, Jolie alitangaza kuwa alikuwa na mimba ya Brad Pitt.[9]

  1. "Brad Pitt". People. Iliwekwa mnamo 12 Machi 2008.
  2. Gliatto, Tom. "Love Lost", 30 Juni 1997. 
  3. "Brad Pitt Biography". People. uk. 2. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-04-24. Iliwekwa mnamo 16 Mei 2008.
  4. * Bandon, Alexandra. Following, Ambivalently, in Mom or Dad's Footsteps. The New York Times. 25 Agosti 1996. Accessed 25 Februari 2009.
  5. Silverman, Stephen M.. "How Will Brad and Angelina's Movie Fare?", People, 21 Januari 2005. Retrieved on 16 Machi 2009. Archived from the original on 2009-06-03. 
  6. Harris, Mark. The Mommy Track. The New York Times. 15 Oktoba 2008. Accessed 18 Oktoba 2008.
  7. "Brad & Angelina's Latest Getaway". People. 4 Mei 2005. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-08-30. Iliwekwa mnamo 16 Mei 2008. {{cite web}}: Cite uses deprecated parameter |authors= (help)
  8. Newcomb, Peter. "Angelina Jolie, Brad Pitt", Vanity Fair, 2 Septemba 2008. Retrieved on 3 Aprili 2009. Archived from the original on 2009-11-30. 
  9. "Angelina Jolie Pregnant". People. 11 Januari 2006. Iliwekwa mnamo 15 Mei 2008.