Blindness (kitabu)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tolea la kwanza katika lugha ya Kireno

Blindness (kwa Kireno: Ensaio sobre a cegueira, maana yake Insha juu ya Upofu) ni kitabu cha riwaya kilichoandikwa na mwandishi wa Kireno anayeitwa Jose Saramago. Kitabu hicho cha riwaya kilitolewa chapa ya kwanza nchini Ureno mwaka 1995, kwa lugha ya Kireno na baadaye mwaka 1997 kilitolewa chapa nyingine kwa lugha ya Kiingereza na hiyo ikiwa ni mwaka 1997. Blindness ni moja kati ya vitabu maarufu vya fasihi pamoja na kitabu cha The Gospel According to Jesus Christ na kitabu cha Baltasar and Blimunda

Mandhari ya riwaya ya Blindness[hariri | hariri chanzo]

Riwaya ya Blindness ni hadithi inayohusisha ugonjwa wa upofu wa kuambukiza ambao haukujulikana chanzo chake ni nini, ugonjwa ambao uliathiri karibu kila mtu katika nchi ya Kusadikika au kufikirika.

Riwaya hii inafuatia inaanza kwa kuelezea jinsi ambavyo ugonjwa wa upofu ulivyoenea kwa kasi kwa kuanzia kwa daktari wa macho ambaye naye aliupata kutoka kwa mgonjwa wa upofu wa kwanza na baadaye ugonjwa huo kuenea kwa wagonjwa wote waliokuwepo katika hospitali aliyokuwa akifanyia kazi daktari huyo na baadaye kuenea nchi nzima isipokuwa kwa mke wa daktari ambaye hadi mwisho wa riwaya hii hakuwahi kuambukizwa ugonjwa wa upofu.

Kufuatia kuenea kwa ugonjwa wa upofu kwa kasi katika nchi hiyo ya kufikirika, kulisababisha machafuko ya kijamii kutokana na kupelekea kukosekana kwa chakula kulikosababishwa na watu wengi kushindwa kuona. Hivyo serikali ya nchi hiyo iliamua kuchukua hatua za kukabiliana na hali hiyo katika nchi yao. Moja kati ya hatua iliyochukuliwa ilikuwa ni kuwatenga watu wote wenye upofu au wenye kuonesha dalili za upofu katika makambi mbali na jamii ambayo haijaathirika na upofu huo.

Hali katika makambi ambayo waliwekwa watu wenye upofu, ambao kwa kundi la kwanza lilijumuisha watu wasiozidi kumi. Ilikuwa siyo nzuri kwani kutokana na vipofu hao hawakupewa ruhusa ya kwenda kuonana na familia zao, lakini mbaya zaidi walitakiwa kujihudumia wenyewe mambo yote ikiwa ni pamoja na kuzikana inapotokea mmoja kati yao kafariki. Lakini kitu pekee cha kuvutia katika riwaya hii, ni kiasi mke wa daktari wa macho alivyoweza kujifanya kuwa katika hali ya upofu na kufanikiwa kuwa na mume wake katika makambi hayo ya vipofu suala lililokuwa msaada mkubwa kwa vipofu wengine hasa wakati wa kuchukua chakula na kufanya shughuli za mazishi.

Sehemu ya kwanza[hariri | hariri chanzo]

Sehemu ya kwanza ya riwaya hii, inaonesha jinsi ambavyo hali ilivyo katika makambi au sehemu za uangalizi maalumu walizowekwa watu waliothirika na upofu. Hali kwa ujumla inaonekana kuwa mbaya. Idadi ya watu inaononekana kuongezeka siku hadi siku, hali ya usafi inazidi kuwa mbaya kutokana na watu wenye upofu hao kushindwa kufanya usafi hasa katika maeneo ya maliwato Kutokana na ukosefu wa chakula katika makambi hayo kunasabisha waathirika hao kushindwa kuvumiliana na kuishi katika hali ya amani, kutoka na kuanza kuisha kwa ushirikiano hali inayosababisha kutokuwa na usawa katika ugawaji wa chakula na uoshaji wa vyomba baada ya kuvitumia.

Wanajeshi[hariri | hariri chanzo]

waliopangiwa kwa ajili ya kulinda waathirikaa hao wanazidi kuwa wakali kutokana na wao kuanza kuathirika na ugonjwa wa upofu mmoja mmoja, Baadae jeshi likaamua kuacha kuwapa dawa baadhi ya waathirika wa upofu waliokuwepo katika makambi hayo ili wafe na hatimaye kumaliza tatizo la upofu nnchini humo. Kwa kuhofia mlipuko zaidi wa ugonjwa wa upofu mwajeshi mmoja anawalipua kundi la vipofu waliokuwa wakisubiria chakula katika makambi hayo Hali ianzidi kuwa mbaya baada ya kundi la wanajeshi kuamua kuingia ndani ya makambi na kuanza kufanya matendo ya kinyama ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa kijinsia kama vile ubakaji kwa waathirika wa upofu.

Baada ya kuzidiwa na njaa ya muda mrefu, waathirika wa upofu waliokuwa wakiishi ndani ya makambi wanaamua kuchoma moto makambi hayo na baada ya kutoka nje ndipo wanagundua kuwa wanajeshi wote walikuwa tayari wamekwisha ondoka hali iliyopelekea waathirika hao kuamua kuondoka katika makambi hayo na kwenda katika jamii waliyokuwa wametengwa nayo na na kukuta hali bado ni mbaya kutokana na watu wote kuwa vipofu hali iliyosababisha hali mbaya ya maisha ikiwa ni pamoja na ukosekanaji mkubwa wa chakula

Baada ya kutoka katika makambi hayo daktari na mke wake pamoja na familia ambayo ilikuwa chini ya uangalizi wa mke wa daktari ambaye bado hadi wakati huo alikuwa bado anaona swala ambalo alilificha na kulifanya siri kwa muda kidogo hapo nyuma Jamii kwa ujumla inaonekana kuvunjika, baada ya upofu kuenea katika familia na shule nyingi. Sheria, utaratibu , huduma za kijamii pamoja na mashule yamefungwa kutokana na jamii nzima kugeuka upofu.

Watu wanaamua kuvamia katika nyumba zilizoachwa bila watu ili kutafuta chakula hali inayosabisha machafuko ya kijamii kutokana na watu kutokuwa na makazi maalumu wala chakula. Daktari na mke wake pamoja na familia yao mpya, tayari wanaanza maisha yao mapya katika moja ya nyumba zilizoachwa na familia zilizoathirika na upofu=, huku wakimtegemea mke wa daktari kwa asilimia kubwa katika maisha yao.

Wahusika[hariri | hariri chanzo]

Mwandishi wa Riwaya ya Blindness Jose saramago ametumia sanaa kwa kiasi kikubwa kwa pamoja na kuwa na uwezo wa kuandika riwaya yenye kuvutia lakini halikadhalika yenye kufundisha, ameweza kuandika riwaya hii bila kutumia jina kamili kwa mhusika hata mmoja kwani majina a wahusika wake amewaita kulingana na kazi au nafasi walizonazo katika riwaya hii. Baadhi ya wahusika katika riwaya hii wako kama ifutavyo. Mke wa daktari ( The doctor’s wife) Huyu ni mke wa daktari wa macho, mtu pekee aliishi katikati ya vipofu wenye kuambukizana bila kupata maambukizo ya upofu huo. Baada ya janga la upofu kuivamia nchi yao na kuathiriri watu wa nchi hiyo kwa kiaisi kikubwa sana, mke wa daktari anafanikiwa kujifanya kama na yeye pia ameathirika na ugonjwa huo ili aweze kupata nafasi ya kwenda kumtunza mume wake katika kambi ya watu wenye upofu.

Mke wa Daktari anatarajia kupoteza uwezo wake wa kupona wakati wowote lakini hali inakuwa si hivyo kwani mke huyo wa dakari anaendelea kuona kwa wakati wote ambapo watu katika nchi nzima walikuwa wameathirika na ugonjwa wa upofu. Katika sehemu ya pili ya riwaya hiyo inayoitwa “seeing” kwa kiswahili “kuona” mke wa daktari anaendelea na uwezo wake wa kuona hali inayosababisha jamii ya watu wengiinupoteza imani nae na kuwa na wasiwasi kuwa kwa nini yeye pekee nchi nzima ndiye aliebaki bila kuwa ameathirwa na ugonjwa wa upofu.

Daktari[hariri | hariri chanzo]

Huyu ni daktari mwenye utaalamua macho, ni mkarimu ambaye nae anapata maambukizi ya ugonjwa wa upofu mara baada ya kujari kutoa matibabu kwa baadhi ya watu wenye upofu. Yeye pamoja na mkewe wanawekwa katika makambi ya vipofu huku mke wake akiendelea kuficha swala la kuwa yeye ana uwezo wa kuona kwa kuhofia kuwa mtumwa katika kambi ya vipofu. Anachaguliwa kuwa kiongozi katika wodi ya vipofu ambapo anajitahidi kadiri ya uwezo wake kuweka wodi katika hali ya usafi na kuweka sheria za usawa katika wodi lakini kutokana na upole wake anajikuta katika hali ngumu kutokana na wagonjwa wa upofu kuwa wengi na kuanza kuleta fujo katika kambi hiyo Msichana mwenye miwani. (Girl With Dark Glasses) huyu ni msichana ndogo mwenye umri wa kadiri ya miaka kumi na ambaye anafanya biashara ya ngono, huyu anapata ugonjwa wa upofu baada ya kufanya mapenzi na moja ya watu ambao waliathirika na ugonjwa wa upofu na yeye pia kama ilivyo kwa waathirika wengine anapelekwa katika kambi za watu wenye ulemavu. Japo kwa asili huyu msichana mwenye miwani myeusi ni mkali na mtu mwenye roho mbaya, kidogo kidogo anaanza kujifunza kuwa mkarimu na mwenye moyo wa upole na upendo baada ya kumtunza mtoto yatima ambaye aliletwa katika makambi hayo kutokana na kupata upofu. Hadi kufikia mwishoni mwa Riwaya hii, Msichana mwenye miwani myeusi anabadilika na kuwa msichana mwenye heshima na tabia nzuri kiasi cha mke wa daktari kumsifia kuwa yeye ni msichana mwenye tabia nzuri.

Mfalme wa wodi namba tatu. Huyu ni kiongozi wa wodi namba tatu, ambaye yeye ni mkali na mwenye asira kwani anawatishia wakazi wengine katika wodi hiyo kwa kutumia bunduki, halikadhalika anawanyima chakula kwani anafikia hatua ya kuhitaji vitu vya thamani kutoka kwao ili aweze kuwapa chakula na inapofikia hatua kuwa vitu vya thami vimekwisha anahitaji wanawake kwa ajili ya kutaka kufanya nao mapenzi, lakini baada ya mwanamke kuuwawa na huyu mlinzi mwenye asira, mke wa daktari nae anaamua kumuua huyo mlinzi. Kifo cha huyu kinasababisha kuungua moto kwa kambi hii ya watu wenye upofu na walinzi wote kupotea kusikojulikana Mwanaume mwenye kovu katika jicho. Huyu mwanaume mzee lakini mpole, ambaye tofauti na wenziwe hakupata mshtuko kufuatia kupata ugonjwa wa upofu ulioivamia nchi yao, Mzee huyu anaendelea kuwapa watu wenye upofu katika makambi hayo taarifa zinazoendelea nje ya makambi kupitia katika redio yake. Ni mtu mwenye imani ya dini sana. Na baada ya uginjwa wa upofu kuisha katika nchi yao,Mzee huyu anasema anatumaini kuwa watu watakuwa wamejifunza kuhusu asili ya binadabu kutokana na ugonjwa huo.

Hitimisho[hariri | hariri chanzo]

Kama zilivyo kazi nyingi za Jose Saramago, riwaya hii inajumuisha sentensi ndefu ambazo si rahisi kupata nafasi ya kuvuta pumzi, wakati mweingine alama ya koma huweza kuwa kama vile inawakilisha alama ya nukta, Kukosekana kwa alama za kufunga na kufungua semi katika sentensi zenye maneno ya majibizano, lakini hali kadhalika kwahusika katika Riwaya hii ya Blindness hawana majina halisi, hii ikiwa inajitokeza kwa wingi sana katika riwaya za Jose Saramago mfano Riwaya ya All the Names au The Cave na pengine hii ndio hasa sanaa au ujuzi katika utungaji wa Riwaya unaomtofautisha Mwandishi wa tamthilia hii na waandishi wengine. Majina yote katika Riwaya hii yanatokana na nafasi walizonazo wahusika, kwa mfano mke wa daktari aliitwa mke wa daktari, mtu wa kwanza kuwa kipofu aliitwa, mtu wa kwanza kuwa kipofu, Nchi au hata mkoa iliyopatwa na ugonjwa wa upofu haikuwahi kutajwa, lakini baadhi, ya vitu alivovitaja katika riwaya yake hii kama vile chakula cha Chouriko, spicy sausagepamoja na maongezi yanayoonekana kuwa na asili ya ureno, yanaonesha kuwa na dalili za kuwepo kwa uwezekano kuwa nchi ambayo Jose Saramago anaiongelea kuwa ni Ureno. Kutokana na umaarufu wa Riwaya hii ya Blindness, ilitengenezwa filamu inayotokana na Riwaya hii, ambayo Mwongozaji wake Fernando Meirelles, ambapo utengenazaji wa wa filamu hiyo ulianza rasmi Mwezi wa saba mwaka 2007 na kuzinduliwa rasmi mwaka 2008.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu: