Bebo Norman

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bebo Norman

Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Jeffrey Stephen Norman
Amezaliwa (1973-05-29)Mei 29, 1973
Columbus, Georgia
Aina ya muziki Nyimbo za kisasa za Kikristo
Kazi yake Mwanamuziki
Ala Gitaa
Tovuti Tovuti Rasmi

Jeffrey Stephen "Bebo" Norman (aliyezaliwa 29 Mei 1973) ni mwanamuziki wa kisasa wa Kikristo kutoka mji wa Columbus, Georgia. Albamu yake ya mafanikio mengi hadi sasa ni Myself When I Am Real, ambayo ina nyimbo maarufu kama "Great Light of the World" na "Falling Down". Nyimbo nyingine za Norman ni "Disappear", "Nothing Without You", "I Will Lift My Eyes", na "Borrow Mine". Yeye,hapo mwanzoni,alipata umaarufu wakati alipozuru na bendi ya Kikristo,Caedmon's Call. Mashabiki wa Norman wanajiita Simpletons.

Norman alikuwa,hapo awali,akihusika katika Young Life Ministries na alipata mashabiki wengi akiwatumbuiza katika makambi ya vijana ya Kikristo. Hii inafuatana kisambamba na wanamuziki Matt Wertz na mwandalizi wa muziki Ed Cash(Chris Tomlin,Amy Grant),ambao walipata umaarufu wao kwa kupitia Young Life. Alipotoa albamu yake Big Blue Sky,albamu ya tatu,Norman aliongeza waraka akiombea michango kwa shirika hilo lao. Wimbo wake waWalk Down This Mountain ni kuhusu matukio yaliyomfanyikia akiwa shamba la Young Life Wilderness Ranch.

Norman alitoa Between the Dreaming and Coming True mnamo Septemba 2006. Ziara ya kupigia debe albamu hii ilishirikisha waimbaji wageni wa Kikristo Aaron Shust na Brandon Heath. Norman ni msomi kutoka Chuo cha Presbyterian huko Clinton, South Carolina.

Wimbo wake, To Find My Way To You ilitumika kwa njia mbalimbali ili kutangaza kuhusu kipindi cha CBS , The Class.

Norman alimwoa Roshare Finecey.

Wimbo mpya wa Bebo ya 2008 inaitwa "Britney" na imeandikwa kwa mwimbaji Britney Spears. (2007-2008),Bebo ameonekana dhahiri mara kadhaa na wasanii maarufu wa Kikristo katika ziara za kuandaa matamasha ya Behold the Lamb ya Andrew Peterson wakati wa msimu wa Krismasi msimu.

Diskografia[hariri | hariri chanzo]

  1. * The Fabric of Verse (1996)
  2. * Ten Thousand Days (1999)
  3. * Big Blue Sky (2001)
  4. * Myself When I Am Real (2002)
  5. * Try (2004)
  6. * Between the Dreaming and the Coming True (2006)
  7. * Great Light of the World: The Best of Bebo Norman (2007)
  8. * Christmas... From the Realms of Glory (2007)
  9. * Bebo Norman (2008)

Tuzo[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Historia ya Tuzo za Dove:Bebo Norman. Gospel Music Association. Jalada kutoka ya awali juu ya 2012-06-05. Iliwekwa mnamo 13 Septemba 2009.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]