Bavelile Hlongwa
Bavelile Gloria Hlongwa (14 Aprili 1981 - 13 Septemba 2019) alikuwa mhandisi wa kemikali wa Afrika Kusini na mwanasiasa kutoka KwaZulu-Natal na mwanachama wa chama cha African National Congress (ANC). Alikuwa Naibu Waziri wa Rasilimali za Madini na Nishati na Mbunge wa Bunge la Afrika Kusini kuanzia Mei 2019 hadi kifo chake Septemba 2019. [1] [2] [3]
Maisha ya mapema na kazi
[hariri | hariri chanzo]Bavelile Gloria Hlongwa alizaliwa 4 Aprili 1981 katika mji wa Umzinto katika Mkoa wa Natal. Alianza masomo yake Shule ya Msingi ya Ncazuka mwaka 1989 na akahitimu kutoka Shule ya Upili ya Sihle mwaka 2000. Alisoma Chuo Kikuu cha KwaZulu-Natal kampasi ya Chuo cha Howard na kupata shahada ya uzamili ya Sayansi katika uhandisi wa kemikali . Akiwa chuo kikuu, Hlongwa alijishughulisha na Umoja wa Vijana wa ANC na mashirika mengine ya wanafunzi. Alikuwa akisoma shahada ya uzamili katika utawala wa umma kabla ya kufaiki kwake. [4]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Deputy Mineral Resources Minister Bavelile Hlongwa dies Ilihifadhiwa 16 Aprili 2022 kwenye Wayback Machine., Johannesburg, eNCA, 14 September 2019. Retrieved on 14 September 2019.
- ↑ Ramaphosa 'shocked and saddened' by Deputy Minister Hlongwa's death, The Citizen, 14 September 2019. Retrieved on 14 September 2019.
- ↑ Somdyala, Kamva. Deputy minister Hlongwa was assisting overturned vehicle when she died, News24, 14 September 2019. Retrieved on 14 September 2019.
- ↑ Bavelile Hlongwa: Deputy Minister of minerals and energy dies in car crash, The South African, 14 September 2019. Retrieved on 14 September 2019.
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Bavelile Hlongwa kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |