Bata-miti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bata-miti
Bata-miti uso-mweupe
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Anseriformes (Ndege kama bata)
Familia: Anatidae (Ndege walio na mnasaba na bata)
Nusufamilia: Dendrocygninae
Reichenbach, 1853
Jenasi: Dendrocygna
Swainson, 1837
Ngazi za chini

Spishi 8:

Mabata-miti au Dendrocygninae ni nusufamilia ya familia ya Anatidae yenye jenasi moja tu, Dendrocygna. Waainishaji wengine wanawaweka ndani ya familia yao wenyewe Dendrocygnidae au ndani ya kabila Dendrocygnini ya familia ndogo Anserinae. Leo kuna spishi nane za mabata-miti na visukuku vya spishi ingine vimefunuliwa kisiwani kwa Aitutaki, Visiwa vya Cook. Wanaitwa mabata-miti kwa sababu hujenga matago yao pengine ndani ya miti. Lakini kwa Kiingereza wanaitwa “whistling ducks” sikuhizi kwa sababu ya sauti yao kama mluzi. Mabata hawa wanatokea popote kwa kanda za tropiki na nusu-tropiki. Wana miguu mirefu na shingo refu na wanapenda kuwa pamoja. Makundi makubwa ya ndege hawa huonekana maziwani.

Spishi za Afrika[hariri | hariri chanzo]

Spishi za mabara mengine[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]