Bas
Bas | |
---|---|
| |
Maelezo ya awali | |
Amezaliwa | Mei 27 1987 |
Asili yake | Paris France |
Miaka ya kazi | 2011–mpaka sasa |
Studio | Dreamville Records |
Abbas Hamad (jina lake la kisanii: Bas; alizaliwa Paris, Ufaransa, 1987) ni mwanamuziki mwenye asili ya Sudani, anayetoka mji wa Queens, jimbo la New York.
Bas amesainiwa kwa lebo ya J Cole, Dreamville Records na Interscope Records.
Albamu yake ya kwanza ya studio, Last Winter, ilitolewa tarehe 29 April, 2014. Albamu yake ya pili ya studio ilitolewa tarehe 4 Machi 2016 na iliitwa Too High to Riot, na albamu ya tatu ni Milky Way na ilitolewa tarehe 24 Agosti 2018.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Yeye alizaliwa katika mji wa Paris 1987 kwa wazazi wa wasudani. akiwa na umri wa miaka nane familia yake ilihamia mji wa New York City jimbo la New York. Yeye alikwenda St. Fracis Preparatory School katika mji wa Queens jimbo la New York.
Bas ni mdogo wa rafiki wa J Cole na meneja Ibrahim Hamad.
Kazi ya Muziki
[hariri | hariri chanzo]Mnamo mwaka 2011, Bas alitoa mixtape yake ya kwanza iliyoitwa “Quarter Water Raised Vol. 1. Mnamo mwaka 2013, miztape yake ya pili ilitolewa na kuitwa, “ Quarter Water Raised Vol. 2.
Mnamo Mwaka 2013 Bas alikuwa kwenye wimbo wa J Cole “New York Times” na pia 50 Cent mpaka albamu J Cole, Born Sinner, na kisha tena katika DJ Khaled “Hells Kitchen” toka Suffering from Success.
Kisha yeye alionekana kwenye albamu Revenge of the Dreamers.” Hiyo mixtape iliyotolewa kusherehekea Dreamville alishirikiana na Interscope Records, matokeo yake ilisainiwa na Interscope. Wiki mbili kabla ya albamu yake ya kwanza “Last Winter”, Bas alitolewa EP ya bure inayoitwa “Two Weeks Notice.”
2014–15: Last Winter
[hariri | hariri chanzo]Last Winter ilitolewa tarehe 29 Aprili 2014, kwa Dreamville records na Interscope Records. Albamu hii ilizungumza kuhusu siku za baridi huko New York wakati yeye alikuwa anarekodi hiyo albamu. Albamu iliungwa mkono na wimbo “My Nigga Just Made Bail” kuunda kwa GP808 na J Cole aliimba kwenye wimbo. Last Winter kutolewa mia na tatu katika orodha Billboard 200 na yeye aliuza nakala 3601 katika wiki za kwanza.
Baada ya kutolewa, Bas alikwenda katika safari ya tamasha la majiji kumi lililoitwa “The Last Winter Tour.” Bas baada ya safari yake ya muziki, alikwenda katika safari ya kimataifa ya muziki kwa Ab Soul. Mnamo mwaka 2015 Bas alikwenda katika safari ya kimtaifa ya muziki na J Cole kwenye “2014 Forest Hills Drive Tour” na wasanii wengine kama Omen, Cozz, Jeremih, YG, na Big Sean.
2016-17: Too High to Riot
[hariri | hariri chanzo]Bas alitoa albamu ya pili, Too High to Riot tarehe 4 Machi 2016. Albamu hii pia inajumuisha kuonekana kwa mgeni kutoka wasanii Dreamvile J. Cole na Cozz. Too High to Riot ilishika nambari arobaini na sita kwenye Billboard 200, na Albamu aliuza nakala 10985 katika wiki za kwanza. Yeye pia alitoa video ya muziki ya wimbo wa evry kwenye albamu. Baadaye, Bas alikwenda katika safari ya kimtaifa ya muziki mnamo mwezi Januari mwaka 2016 iliyoitwa “The Too High to Riot Tour.”Wasanii wa Dreamville Cozz na Earthgang alikwenda safari na walikwenda waji ishirini na sita, na tarehe 29 Januari 2017 video inayofunika safari ilitolewa katika Tidal.
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Bas kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |