Barbara Ayisi Asher
| Barbara Ayisi Asher | |
| Amezaliwa | 12 Februari 1976 Ghana |
|---|---|
| Nchi | Ghana |
| Kazi yake | mwanasiasa |
Barbara Ayisi Asher (alizaliwa 12 Februari, 1976) ni mwanasiasa wa nchini Ghana na Mbunge wa zamani wa Jimbo la Cape Coast Kaskazini katika mkoa wa kati wa Ghana[1].
Pia yeye ni mwanachama wa chama cha siasa cha New Patriotic Party na alikuwa naibu waziri wa zamani wa Elimu nchini Ghana[2].
Aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Ligi Kuu ya Wanawake ya Super Cup ya Mitaa (LOC)[3].
Maisha yake na Elimu
[hariri | hariri chanzo]Barbara Asher Ayisi alizaliwa tarehe 12 Februari 1976 huko Effutu, Mkoa wa Central, Ghana. Yeye ni mhitimu wa Chuo cha Ualimu cha Our Lady of Apostles (OLA) na Chuo Kikuu cha Elimu, Winneba. Ana shahada ya uzamili katika Fasihi ya Kiingereza kutoka Chuo Kikuu cha Cape Coast.[4][5]
Historia ya kazi
[hariri | hariri chanzo]Kabla ya kuchaguliwa kuwa mbunge, alifanya kazi kama mlezi wa darasa (form mistress) kati ya mwaka 2003 na 2006 katika Huduma ya Elimu ya Ghana (GES), na pia kama mlezi wa bweni (housemistress) kuanzia mwaka 2010 hadi 2016 katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Wesley.[6]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-10-22. Iliwekwa mnamo 2022-03-12.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-10-22. Iliwekwa mnamo 2022-03-12.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-10-23. Iliwekwa mnamo 2022-03-12.
- ↑ https://ghanamps.com/mps/details.php/?id=5353
- ↑ https://web.archive.org/web/20230921230933/https://www.parliament.gh/mps?mp=95
- ↑ https://web.archive.org/web/20240226202704/https://ghanaelections.peacefmonline.com/pages/2016/central/cape_coast_north/
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Barbara Ayisi Asher kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |