Nenda kwa yaliyomo

Bandari ya Mtwara

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bandari ya Mtwara

Bandari ya Mtwara ilijengwa wakati wa ukoloni wa Waingereza katika Jiji la Mtwara, kusini mwa nchi ya Tanzania ya leo.

Historia ya bandari[hariri | hariri chanzo]

Bandari ya Mtwara iliimarishwa wakati wa ukoloni na Waingereza mnamo miaka ya 1948-1954, na reli ilijengwa ikiunganisha bandari hiyo, kama sehemu ya Mradi wa Karanga wa Tanganyika. Kwa sababu ya kutokufanikiwa  kwa mradi huo bandari hiyo ilipoteza thamani yake na reli iliondolewa.

Bandari hiyo ilikuwa ikifanya kazi lakini haikutumika sana kwa miaka mingi kutokana na miundo mbinu mibovu ya uchukuzi,[1] Lakini, katika miaka ya 2010-2011 kutokana na  kuongezeka kwa shughuli katika utaftaji wa rasilimali ya mafuta na gesi, shughuli za bandari ziliongezeka.[2]

Uendeshaji[hariri | hariri chanzo]

Bandari imeshughulikia shehena kidogo sana kutokana na kukosekana kwa viwanda vikubwa katika eneo hilo. Uuzaji mkubwa wa nje ya bandari umekuwa ni zao la korosho kila mara. Bandari ina ukuta wa mita 385.[3] Hapo awali bandari hiyo ingeweza kupokea meli 2 za urefu hadi mita 175. Tangu ukarabati wa mwaka 2015, bandari hiyo inaweza kushughulika pia meli ya mita 209.[4] Bandari hiyo inashughulikia tani 400,000 za mizigo  kila mwaka ambazo ni chini ya  asilimia 5 (5%)  ya jumla za shehena za nchi, hata hivyo, serikali imepanga kuboresha bandari hiyo zaidi ili kuwezesha biashara katika sehemu ya kusini mwa  nchi.[5].

Mipango[hariri | hariri chanzo]

Bandari ya Mtwara pia ni sehemu muhimu ya mradi wa "Mtwara Development Corridor" na hivi karibuni yamefanyika maboresho makubwa.[5].Bandari pia ina eneo maalum la kiuchumi lililounganishwa na bandari hiyo.Mnamo Desemba mwaka 2015 "Alistair Freeports Limited" iliingiza  dola ($) 700,000 kuboresha "eneo la usindikaji" karibu na eneo la bandari.[6].

Ona pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. TPA, TPA Ports, Mtwara Archived 2012-02-19 at the Wayback Machine
  2. The Economist - Tanzania’s gas boom - The Mtwara Rockefellers
  3. "MTWARA PORT". www.tanzaniaports.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-09-02. Iliwekwa mnamo 2015-12-31. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
  4. "Tanzania: Mtwara Port Handles Huge Ships After Renovations". allAfrica.com. Allafrica. Iliwekwa mnamo 2015-12-31.
  5. 5.0 5.1 "Mtwara port set for major upgrade". www.theeastafrican.co.ke. Iliwekwa mnamo 2015-12-31.
  6. "Dar Firm Injects Sh1.5 Billion in Mtwara's Free Port Zone", AllAfrica, 21 December 2015.