Bandari ya Sydney

Bandari ya Sydney (pia inajulikana kama Bandari ya Jackson) ni bandari ya asili iliyoko katika pwani ya Mashariki mwa Australia, ndani ya jiji la Sydney. Bandari hii ipo karibu na maeneo maarufu kama Jumba la Sanaa la Sydney na Daraja la Bandari ya Sydney.[1]
Historia
[hariri | hariri chanzo]Kabla ya kufika kwa walowezi wa Ulaya, eneo lililozungukwa na Bandari ya Sydney lilikuwa makazi ya kabila fulani la Aboriginal, ambalo lilijumuisha makabila madogo madogo kama Gadigal, Cammeraygal, Eora, na Wanegal.
Inaaminika kwamba kabila la Gadigal hapo awali liliishi katika eneo la kusini mwa Bandari ya Jackson, huku kaskazini mwa bandari likiwa makazi ya Cammeraygal. Eneo la upande wa kusini mwa Mto Parramatta, ambalo ni magharibi mwa Petersham hadi eneo la Rose Hill, lilimilikiwa na kabila la Wanegal. Kabila la Eora liliishi upande wa kusini mwa bandari, karibu na eneo ambapo walowezi wa kwanza wa Ulaya waliweka kambi yao ya mwanzo.[2][3]
Visiwa
[hariri | hariri chanzo]Bandari ya Sydney ina visiwa vingi vya asili, ikiwa ni pamoja na: Kisiwa cha Shark, Kisiwa cha Clark, Fort Denison, Kisiwa cha Mbuzi, Kisiwa cha Cockatoo, Kisiwa cha Spectacle, Kisiwa cha Snapper,na Kisiwa cha Rodd . Visiwa vingine vya zamani ni Kisiwa cha Bennelong , Kisiwa cha Garden, na Kisiwa cha Berry , ambavyo vimeunganishwa na nchi kavu kupitia madaraja yaliyopo.[4]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Brown, Robert (1810). Prodromus floræ Novæ Hollandiæ et Insulæ Van-Diemen : exhibens characteres plantarum quas annis 1802–1805 /. Londini: typis R. Taylor et socii.
- ↑ "Sydney Harbour National Park". NSW National Parks.
- ↑ "Rolex Sydney Hobart Yacht Race 2024". rolexsydneyhobart.com. Iliwekwa mnamo 2024-06-27.
- ↑ Mayer-Pinto, M.; Johnston, E. L.; Hutchings, P. A.; Marzinelli, E. M.; Ahyong, S. T.; Birch, G.; Booth, D. J.; Creese, R. G.; Doblin, M. A.; Figueira, W.; Gribben, P. E.; Pritchard, T.; Roughan, Steinberg; Steinberg, P. D.; Hedge, L. H. (2015). "Sydney Harbour: a review of anthropogenic impacts on the biodiversity and ecosystem function of one of the world's largest natural harbours" (PDF). Marine and Freshwater Research. 66: 1088–1105. doi:10.1071/MF15157. Iliwekwa mnamo 10 Februari 2024.
{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
| Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |