Bandari ya Sydney

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha inayoonyesha Jumba la Sanaa la Sydney na Daraja la Bandari ya Sydney.

Bandari ya Sydney (pia inaitwa Bandari ya Jackson) ni bandari asilia. Ipo katika pwani ya Mashariki mwa Australia katika Sydney. Bandari ya Sydney pia ipo katika eneo maarufu ya Jumba la Sanaa la Sydney na Daraja la Bandari ya Sydney.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Kabla kufika kwa walowezi wa kutoka Ulaya, eneo lilozungukwa na Bandari ya Sydney ilikuwa makazi ya kabila fulani liitwalo aboriginal, kabila limebeba makabila mengine madogo madogo kama vile Gadigal, Cammeraygal, Eora na kabila la Wanegal.

Inaaminika kwamba watu wa kabila la Gadigal hapo awali walianza kuishi katika eneo la upande wa kusini mwa Bandari ya Jackson. Na Kaskazini mwa Bandari ya Sydney yasemekana kuwa kabila Cammeraygal lilikuwa linaishi huko. Pia yaaminika kwamba eneo la upande wa Kusini wa Mto Parramatta, yaani magharibi mwa Petersham na kutokezea kule kunakoitwa Rose Hill, kulikuwa kukimilikiwa na kabila la Wanegal. Kabila la Eora waliiishi upande wa Kusini mwa Bandari ya Sydney, ambapo si mabli sana na sehemu ya kwanza ya walowezi kuweka kambi yao.

Visiwa[hariri | hariri chanzo]

Kuna visiwa chungu nzima katika Bandari ya Sydney, visiwa hivyo ni kama ifutavyo: Shark Island, Clark Island, Fort Denison, Goat Island, Cockatoo Island, Spectacle Island, Snapper Island na Rodd Island. Baadhi ya visiwa vya zamani: Bennelong Island, Garden Island na Berry Island ambacho kimeungana na nchi kavu kwasababu ya daraja liliopo.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. NSW Govt Printer (1892), Historical Records of New South Wales, Vol 1, Part 2 (1783-1792) pages 67-70.