Bamvua (mnyama)
Mandhari
Bamvua | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Bamvua wa wayo (Lepeophtheirus pectoralis)
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Jenasi 37; zile kubwa zaidi: |
Bamvua ni gegereka wadogo wa familia Galigidae katika ngeli Maxillopoda. Kuna spishi 559 katika jenasi 37. Jenasi kubwa zaidi ni Caligus yenye spishi 268 na Lepeophtheirus yenye spishi 162. Bamvua ni vidusia wa nje ambao wanakula ute, tishu ya epidermi na damu za samaki wa bahari waliotumika kama mlisha. Vidusia hawa wanaweza kuwa shida kubwa katika ufugaji wa samaki, k.m. ule wa samoni katika bahari.
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Bamvua wa samoni
-
Bamvua mgongoni kwa samoni anayefugwa