Nenda kwa yaliyomo

Bamba la Nazca

Majiranukta: 15°00′00″S 85°00′00″W / 15.00000°S 85.00000°W / -15.00000; -85.00000
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bamba la Nazca

Bamba la Nazca ni moja kati ya mabamba ya gandunia yaani mapande ya miamba yanayounda ganda la Dunia. Bamba hilo limepokea jina lake kutokana na mji wa bandari wa Peru wa Nazca.

Bamba la Nazca liko mbele ya pwani la magharibi la Amerika Kusini. Ni moja ya mabamba yanayofunikwa kabisa na bahari, isipokuwa kuna visiwa vichache, kama Visiwa vya Juan Fernández. Eneo lake ni takribani kilomita za mraba 15,600,000[1].

Bamba hilo lina mwendo kuelekea polepole upande wa mashariki, linapogongana na bamba la Amerika Kusini ambalo ni bamba la kibara.

Katika mgongano huo bamba la Nazca lilisukumwa chini ya bara la Amerika Kusini na kuzama hapo kwenye koti la Dunia.

Tabia ya kawaida ya maeneo hayo ni matetemeko ya ardhi ya kina kirefu cheye vitovu vya mita mia kadhaa[2].

Kwenye mpaka ambako bamba moja linazama hutokea mifereji ya bahari kama vile Mfereji wa Atacama (kina hadi mita 8,065) na Mfereji wa Peru (kina hadi m 6369). Wakati huohuo, bara la Amerika Kusini liliinuliwa. Kama matokeo ya kusogezwa kwa mabamba milima ya Andes ilikunjwa kwenye pwani ya magharibi ya Amerika Kusini hadi kimo cha mita 6,962.

Kwa upande wa kaskazini, bamba la Nazca linapakana na bamba la Cocos, upande wa magharibi na bamba la Pasifiki na upande wa kusini na bamba la Antaktiki. Kwenye mashariki, linakutana na bara la Amerika Kusini likizama chini yake.

  1. "Sizes of Tectonic or Lithospheric Plates". About.com Geology. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-06-05. Iliwekwa mnamo 4 Januari 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Darwin Gap quake will shake Chile again [1], New Scientist, 30 Jan 2011, accessed 8 Feb 2011.

Marejeo mengine

[hariri | hariri chanzo]

15°00′00″S 85°00′00″W / 15.00000°S 85.00000°W / -15.00000; -85.00000