Baada ya Jumamosi yaja Jumapili

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Baada ya Jumamosi yaja Jumapili (kwa Kiarabu: min sallaf es-sabt lāqā el-hadd qiddāmūh, kwa tafsiri ya neno kwa neno, 'Ikimpita Jumamosi, ataipata Jumapili') ni methali ya Mashariki ya Kati. Imewekwa kwenye kumbukumbu nchini Misri, Shamu na Lebanoni, ingawa katika utofauti: 'Mkope Jumamosi, ukabiliwe na Jumapili'.

Kwa mujibu wa maelezo ya baadhi ya waandishi, methali hiyo ni maarufu miongoni mwa Wamaroni ambapo maana yake ni Waislamu watawafukuza Wakristo baada ya kuwashughulikia Wayahudi, ikimaanisha kuna lengo la baadaye la kuzifuta au kuzifukuza jamii za wachache kutoka kwenye ulimwengu wa Waislamu.

Mwanahekaya wa Kiizraili, Shimon Khayyat ameitafsiri kama ujumbe wenye tishio, akidai: "Kwa kuwa sasa Wayahudi wanateswa, ujio wa zamu ya Wakristo si jambo la kuepukika kwani ni Jumapili inayoifuatia Jumamosi. Matumizi ya hivi karibuni ya methali hiyo yamehusishwa na Waarabu wa Kikristo na kuleta hisia za kuogofya kuwa muda si mrefu watafukuzwa katika kiwango kitakocholingana na kuondoka kwa Wayahudi kutoka mataifa ambamo Waislamu ndio wengi. Mara kwa mara hukaririwa kwamba methali hiyo hutumiwa na Waislamu wenye misimamo mikali kama kauli mbiu ya kuzitisha jamii enyeji za Kikristo.