Augustine Mulenga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Augustine Kabaso Mulenga (alizaliwa 17 Januari 1990) ni mchezaji wa soka wa Zambia ambaye anacheza katika klabu iliyopo nchini Afrika Kusini iitwayo Orlando Pirates na timu ya taifa ya Zambia.

Kazi ya kilabu[hariri | hariri chanzo]

Mnamo Januari 2018, Mulenga alijiunga na Klabu ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini Orlando Pirates.Alicheza timu hiyo kwa mara ya kwanza 3 Machi 2018, akiingia kama mbadala wa Justin Shonga dakika ya 84 katika ushindi wa 3-1 nyumbani dhidi ya Kaizer Chiefs.

Mulenga alifunga goli lake la kwanza katika klabu hiyo 4 Aprili 2018 katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Bloemfontein Celtic.

Kazi ya Kimataifa[hariri | hariri chanzo]

Alicheza katika kikosi cha timu ya taifa ya Zambia kwa mara ya kwanza mnamo 26 Machi 2017 katika mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Zimbabwe.

Football.svg Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Augustine Mulenga kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.