Auckland Grammar School

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Auckland Grammar School.

Auckland Grammar School ni shule ya umma ya mjini Auckland, New Zealand. Shule inafundisha watoto kuanzia umri wa miaka kumi na tatu hadi kumi na saba. Shule pia ina bweni la kulazia wanafunzi wanaotoka mbali, hivyo ukaa mahali hapo pa shule. Ni moja kati ya mashule makubwa nchini New Zealand. Shule ina zaidi ya wanafunzi elfu mbili. Wito wa shule ni "Per Angusta Ad Augusta: kwa lugha ya kwao". Inamaana ya kwamba "Soma kwa bidii ili upate mafanikio".

Historia ya shule[hariri | hariri chanzo]

Auckland Grammar School ilianzishwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 1868 na Mh. George Grey. Ambaye alikuwa Gavana wa New Zealand toka mwaka 1861 hadi mwaka 1868. Kipindi hicho, kulikuwa na walowezi wapya kutoka Ulaya waliokuwa wakipigana na kabila la Maori juu ya haki ya kumiliki ardhi nchini humo.

Gavana wa New Zealand akaomba msaada wa kijeshi kutoka katika utawala wa Kiingereza ili aweze kutatua tatizo hilo. Kwa bahati Wa-Britain wakatuma karibu wanajeshi milioni moja kwenda kutatua mzozo huo wa ardhi katika New Zealand. Wanajeshi waliowengi waliweka makazi na familia zao katika mji huo wa Auckland. Mh. George Grey akaamua kutengeneza shule ambayo itakayo toa elimu kwa watoto wa wanajeshi walioweka makazo yao katika mji Auckland, na ndipo hapo ilipo anzishwa shule "Auckland Grammar School".

Taratibu za shule[hariri | hariri chanzo]

Watu wa madaraja tofauti au mwenye asili tofauti ambaye anaishi New Zealand wote ni sawa mara tu muda utakapofika yeye kutaka kwenda shule, haito angaliwa kama ni mzawa ama sio mzawa. Shule inaamini kwamba ni vyema kufundisha lugha tofauti, na wanaelekeza kwa kutumia kwa kutumia herufi za Kilatini. Shule inajaribu kuchukua wanafunzi na kuwafunza masomo yenye kueleweka katika nyanja hiyo ya elimu, kuanzia kilimo michezo na kadhalika.

Watu maarufu waliosoma shule hiyo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]