Anup Singh
Anup Singh (amezaliwa Dar es Salaam, Tanzania, 14 Machi 1961) ni mtayarishaji wa filamu anayeishi mjini Geneva, Uswisi.
Amezaliwa katika Afrika ya Mashariki na kukua katika familia ya Sikh yenye asili ya Punjab.[1]
Alihitimu masomo yake ya Fasihi na Falsafa kutoka Chuo cha Bombay na Taasisi ya filamu na runinga huko Pune,India. Aliongoza filamu kwa ajili ya runinga za Kihindi na mshauri katika taasisi ya habari kituo cha BBC na uhakiki wa filamu kwa ajili ya vyombo maalum vya habari. Eki Nadir Naam(Jina la Mto) ambayo ni filamu yake ya kwanza kwa urefu ilichaguliwa kwenye matamasha 30 mbalimbali duniani na ilishinda tuzo kadhaa. Kazi yake ya pili iliyojulikana kwa jina la QISSA- Hadithi ya Mzimu Mpweke (The Tale of a Lonely Ghost) iliyozinduliwa mjini Toronto mnamo mwaka 2013, ambayo ilisifiwa na vyombo vya kimataifa vya habari kwa kuibua hisia nzito na utofauti wake katika usimulizi na mpango wake kwenye hizo simulizi.
Tuzo alizowahi kupata ni Filamu Bora ya Kiasia ya Netpac, Tuzo ya Silver Getaway (The Silver Gateway Award) katika tamasha la filamu la Mumbai. Katika siku za karibuni amekuwa akijishughulisha katika ukamilishaji wa filamu yake ya tatu, The Song of Scorpions (Wimbo wa Nge) inayojumisha waigizaji kama Golshifteh Farahani, Irrfan Khan, Waheeda Rehman na Shashank Arora.[2][3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "The Match Factory". Iliwekwa mnamo 17 Julai 2014.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ cinemas-asie.com - Anup Singh
- ↑ "swissfilms.ch - Anup Singh". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-12-21. Iliwekwa mnamo 2019-12-21.