Anton Chekhov
Anton Pavlovich Chekhov (Kirusi Антон Павлович Чехов; 29 Januari 1860 - 15 Julai 1904) alikuwa mwandishi Mrusi aliyeandika riwaya fupi na tamthiliya.
Early life
[hariri | hariri chanzo]Anton Chekhov alizaliwa mjini Taganrog. Babake alikuwa mwenye duka. Baada ya baba kufilisika familia ilikuwa maskini sana. Anton alilipa masomo yake kwa kufundisha wanafunzi wadogo. Shuleni alisoma mengi pamoja na vitabu vya Miguel de Cervantes na Arthur Schopenhauer. 1879 Chekhov aliweza kujiunga na chuo kikuu cha Moskva alipofuata kozi ya tiba.
Akiwa mwanafunzi alianza kuandika hadithi na riwaya fupifupi kama njia ya kujipatia riziki na kusaidia familia yake. Tangu 1876 gazeti kubwa lilimwagiza kuandika hadithi za mara kwa mara. Kwa njia hii alikufa maarufu na watu wengi walipenda maandishi yake. Aliendelea kutunga pia vitabu na tamthiliya.
1890 Chekhov alifanya ziara kwenda kisiwa cha Sakhalin kilichokuwa gereza akaandika kitabu juu ya hali mbaya ya gereza hili na jinsi gani wafungwa walivyotendewa kwa udharau na unyama.
1892 aliweza kununua ardhi na nyumba mashambani karibu na Moskva. Hapa aliendeela kuandika mengi akisaidia watu maskini walioishi sehemu zile kwa kuwapa chakula na kuwatibu.
1897 aligonjeka akahamia Yalta penye hali ya hewa nzuri zaidi kwa hali yake. Hapa aliendelea kuandika hadi safari yake ya mwisho. Alienda Ujerumani kwa kutibiwa akafa hapo.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Web page A.P. Chekhov Ilihifadhiwa 4 Julai 2010 kwenye Wayback Machine. on a site of the Taganrog Central Public Library named after A. P. Chekhov