Anna Ndege

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Anna Ndege (alizaliwa Shinyanga tarehe 5 Machi 1982) ni mwanariadha Mtanzania aliyeshiriki mashindano ya mbio za urefu wa kati. Ubora wake wa kukimbia umbali wa mita 1500 kwa muda wa dakika 4:09.71. Vilevile ni miongoni mwa Watanzania wanaoshikilia rekodi ya mashindano ya riadha.

Matokeo yake mazuri kuwahi kuyapata yalikuwa ni kushika nafasi ya kumi na tisa katika mashindano ya mbio fupi za mwaka 2001 (IAAF World Cross Country Championships). Ameiwakilisha Tanzania katika mashindano ya jumuiya ya madola mara mbili akiwa anashiriki mbio fupi za wanawake (IAAF World Cross Country Championships – Women's short race 2001 na 2002). Vile vile alishiriki katika mashindano ya jadi ya mwaka 2002 yaani kwa Kiingereza yanaitwa 2002 Commonwealth Games, Alishiriki kukimbia mbio zote za mita mia nane (800) na mita elfu moja mia tano (1500).[1] Alikuwa mshindi mdogo wa medali hizo zilizoshindaniwa (Africa Military Games).[2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Commonwealth Games Athletics. BBC Sport. Retrieved on 2015-01-30.
  2. Africa Military Games. GBR Athletics. Retrieved on 2015-01-30.