Nenda kwa yaliyomo

Angola Avante

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bendera ya Angola
Bendera ya Angola

Angola Avante ("Nenda mbele, Angola") ni wimbo wa taifa wa Angola.

Rui Alberto Vieira Dias Mingas ndiye aliyetunga wimbo huo[1][2], huku mashairi yakitungwa na Manuel Rui Alves Monteiro. Ulipitishwa kama wimbo wa taifa mnamo mwezi Novemba 1975, wakati nchi ilipopata uhuru wake kutoka kwa Ureno. Maneno hayo yanarejelea matukio kadhaa muhimu ya Chama cha People's Movement for the Liberation of Angola (MPLA), ambacho kimekuwa madarakani tangu uhuru na kilikuwa chama pekee nchini Angola hadi mwaka 1992.

  1. "Angola". The World Factbook. CIA. Iliwekwa mnamo Agosti 16, 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Rui Alberto Vieira Dias Mingas". Naxos.com. Naxos Records. Iliwekwa mnamo Agosti 16, 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)