Amiri Sudi Andanenga
Mandhari
Amiri Abdallah Sudi (maarufu kwa jina la kishairi Andanenga au Sauti Ya Kiza; alizaliwa Kilwa tarehe 5 Januari mwaka 1932) ni mshairi wa Kiswahili kutoka Tanzania.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Mwaka 1949 alipelekwa shule ya msingi Kikole hukohuko Kilwa.
Baadaye alisoma shule ya upili ya Songea ambapo kutokana na tatizo la karo alishindwa kuendelea na masomo ya darasa la kumi.
Andanenga alianza kutambulika rasmi katika uwanda wa mashairi mwaka 1954.
Andanenga ameandika vitabu kadhaa ikiwemo kile cha Diwani ya Ustadh kilichotoka mwaka 1997.
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Amiri Sudi Andanenga kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |