Nenda kwa yaliyomo

Amelia Kajumulo Kivaisi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Amelia Kajumulo Kivaisi
UtaifaMtanzania
Majina mengine Profesa Amelia
Kazi yakeMkufunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, Mjasiliamali, Mtafiti

Amelia Kajumulo Kivaisi ni profesa mstaafu wa mikrobiolojia tumizi. Alikuwa mwanachama mwanzilishi na mkuu wa kwanza wa Idara ya biolojia ya molekuli (MBB) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambapo amekua profesa kwa takriban miaka 15. Kwa sasa anafanya kazi kwa mkataba katika idara hiyohiyo.[1].

Hivi karibuni ametunukiwa cheo cha profesa "emerita", akiwa kwenye jopo la kwanza la wanataaluma na mwanamke wa kwanza kutunukiwa cheo hicho kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam [2].

Amelia ni msomi ambaye ana elimu za shahada ya pili (MSc) na shahada ya uzamivu (PhD) ya sayansi ya mikrobiolojia na alijikita katika mmeng'enyo anaerobia wa mabaki ya kilimo ya lignicellulosic.

Amelia amekuwa mtafiti kwa miaka mingi, utafiti wake ulilenga ubadilishaji wa kibiolojia wa taka ngumu za kikaboni kuwa gesi ya asilia, uyoga na viuatilifu vya kibilojia. Amesimamia na kushauri wanafunzi wengi wa shahada ya pili (MSc) na shahada ya uzamivu (PhD) na kuongoza miradi kadhaa ya kitaifa na ya kimataifa ya utafiti.

Kwa kushirikiana na washirika wa viwandani, kwa sasa anahusika katika kukuza daraja la biashara-viuatilifu vya kibilojia akiwa kama mhariri mkuu wa Jarida la Sayansi la Tanzania na amechapisha katika majarida kadhaa. Alisambaza zaidi matokeo ya utafiti kupitia ushiriki wa dhati katika mikutano mingi ya kisayansi.

Hii ni orodha ya baadhi ya tafiti na kazi mbalimbali zilizofanywa na Prof. Amelia

Pia amehusika na kutoa marejeo na hariri katika tafiti nyingine zilizofanyika nje ya Tanzania. [8]

  1. https://www.udsm.ac.tz/web/index.php/staff/name/Amelia%20/165
  2. https://www.udsm.ac.tz/web/index.php/offices/aca/professors-emeriti
  3. Food for thought: Food security and entrepreneurship
  4. http://www.mondofungo.it/Non_Green_Revolution.html
  5. https://www.yumpu.com/xx/document/read/11387414/nitapata-wapi-udongo-wa-kupandia-uyoga-uyoga-tanzanian-
  6. http://connection.ebscohost.com/c/articles/87992048/tanzania-sisal-industry-auditing-characterization-sisal-post-harvest-wastes-as-bio-resource-bio-refining
  7. https://europepmc.org/article/MED/26664748?singleResult=true
  8. https://scholar.google.com/citations?user=Rrl9cxwAAAAJ&hl=cs
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Amelia Kajumulo Kivaisi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.