Amelia Earhart
Mandhari
Amelia Earhart | |
---|---|
Amezaliwa | 24 Julai 1897 |
Utaifa | Mmarekani |
Kazi yake | Rubani |
Mwenza | George P. Putnam |
Amelia Mary Earhart (Julai 24, 1897; Januari 5, 1939) alikuwa rubani wa usafiri wa anga wa Marekani[1].
Earhart alikuwa rubani wa kike wa kwanza kuruka peke yake na kuvuka Bahari ya Atlantiki na aliweka rekodi nyingine nyingi[2]. Alikuwa mmoja wa rubani wa ndege wa kwanza kukuza usafiri wa anga kibiashara, aliandika vitabu vilivyouzwa zaidi kuhusu uzoefu wake wa urubani, na alisaidia sana katika uundaji wa shirika la marubani wa kike, lililojulikana kama The Ninety-Nines.
Mnamo Julai 2, 1937, Earhart alitoweka juu ya Bahari ya Pasifiki wakati akijaribu kuwa rubani wa kwanza wa kike kuzunguka Dunia.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Amelia Earhart", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2024-04-28, iliwekwa mnamo 2024-05-06
- ↑ "National Geographic". National Geographic (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-05-06.