Amélie Wabehi
Amélie Wabehi | |
---|---|
Amezaliwa | Amélie Wabehi Zadjé Ivory Coast |
Kazi yake | Mwigizaji na mchekeshaji |
Amélie Wabehi Zadjé ni mwigizaji na mchekeshaji kutoka Ivory Coast.
Wasifu wake
[hariri | hariri chanzo]Wabehi alianza kufanya uigizaji katika michezo ya maigizo ya shule ya msingi, akiigiza kama Sara, mke wa Ibrahimu katika mchezo wa kuigiza wa Kibiblia[1]. Alifanya uigizaji wake wa kitaalamu mnamo mwaka 1992 na kikundi cha Guignols d'Abidjan. Mnamo mwaka 1994, Wabehi aliigiza katika filamu yake ya kwanza ijulikanayo kama Coupable tradition. Aliigiza katika kipindi cha televisheni cha Ma Famille mnamo mwaka 2002.[2] [1] Jukumu lake kama Amélie lilimletea umaarufu nchini Ivory Coast. Mnamo mwaka 2007, Wabehi aliigiza katika tamthilia ya Dragonnier.[1]
Wabehi amefanya kazi kwa karibu na Akissi Delta. Mnamo mwaka 2018, Wabehi alimkosoa Waziri wa Utamaduni wa Ivory Coast, Maurice Bandaman kwa kushindwa kutimiza ahadi yake ya kutoa faranga za CFA, milioni 100 alizoahidiwa Akissi Delta kwa utengenezaji wa filamu.
Wabehi ana mtoto mmoja wa kiume.[2] Yeye ni Mkristo na mara nyingi husoma vifungu vya Biblia ili kutafakari. Wabehi amekosoa sheria ya Ivory Coast dhidi ya uzinzi, akisema kwamba ikiwa mume wake atamdanganya, angejiuliza badala ya kutafuta kifungo kwa ajili yake. [3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 1.2 "Amélie Wouabéï : " Ma priorité, c’est la joie ! "", Lefaso.net, 10 April 2007. (French)
- ↑ 2.0 2.1 "Amélie Wabehi, comédienne ivoirienne, actrice dans la série "Ma Famille": Révélations sur sa vie privée, sa carrière et ses relations avec Delta", L'Evénement Precis, 13 March 2015. Retrieved on 2021-11-07. (French) Archived from the original on 2020-10-29.
- ↑ "Amélie Wabehi (Comédienne): "J'ai quelqu'un dans ma vie..."", Koundaninfos, 6 August 2020. Retrieved on 2021-11-07. (French) Archived from the original on 2021-11-07.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Amélie Wabehi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |