Ally Rehmtullah
Ally Rehmtullah (alizaliwa Januari 18 1986) ni mbunifu wa mitindo wa Kitanzania [1].
Maisha ya awali na kazi[hariri | hariri chanzo]
Ni mtanzania wa kizazi cha nne mwenye asili ya Kihindi, ambaye alisoma katika shule ya Sanaa ya Baum na chuo cha Lehigh Valley Marekani[2] kabla ya kurejea Tanzania kufanya kazi kama mwalimu wa sanaa ya picha mpaka alipobadili taaluma yake hadi kwenye ubunifu wa mitindo[3]. Mnamo Septemba 2008, alikua mbunifu wa kwanza wa Afrika Mashariki kufanya maonyesho ya mavazi katika London Fashion Week.