Nenda kwa yaliyomo

Alain Makaba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Alain Makaba (amezaliwa 29 Aprili, 1968 mjini Kinshasa) ni mwimbaji, mwandishi wa nyimbo, mpangaji wa muziki, na mpiga gitaa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Anajulikana kama mmoja wa waanzilishi wa kundi la muziki la Wenge Musica.

Alain Makaba Kayele ni mtoto wa Clément Makaba Kayele na Hélène Matapa. Alisoma katika shule ya bweni ya Kikatoliki ya Notre-Dame de Mbanza-Boma iliyopo katika eneo la Bas-Congo ambako alijifunza kupiga gitaa kutoka kwa marafiki zake wa Wenge Musica, akiwemo Didier Masela, Zing Zong, Aime Bwanga, Dédé Masolo, na Werrason.

Mnamo mwaka 1986, mpiga gitaa Zing Zong aliondoka kuelekea Ulaya kulimpa kete ya kwanza Alain Makaba katika kundi hilo. Alijifunza mbinu za upangaji kwenye kinanda katika kundi lake la Bobongo Stars kupitia Studio ya Bobongo pamoja na Al Nzimbi na Shakara Mutela. Kundi hilo lilirekodi albamu yake ya kwanza Bouger Bouger Makinzu. Makaba alitunga wimbo wake wa kwanza uliotolewa, Fisol, na baadaye akawa Mkurugenzi wa Sanaa wa kundi hilo.

Miaka mitatu baadaye, mnamo 1991, alitoa albamu ya pili Kin é Bouge, yenye nyimbo tano. Ndani yake alitunga wimbo Princesse Pathy. Wimbo ambao aliomwandikia mpenzi wake wa wakati huo Bi. Patricia Longomba. Dada wa mpiga ngoma wa wakati huo Awilo Longomba. Baadaye alisafiri kwenda Ulaya kusoma upigaji muziki wa jazz.

Mnamo mwaka 1992, walirekodi albamu Pleins Feux ambayo ilitolewa mwaka 1996. Aliandika upya wimbo wake Fisol, na kuuita La Vie.

Mwaka 1993, kundi lilirekodi na kutoa moja ya kitu kilichoitwa mafanikio makubwa katika historia ya kundi hilo kwa wakati huo. Walitoa albamu ya tatu yenye jina Kala-Yi-Boeing. Albamu ilikuwa na nyimbo saba. Humo ndani alitunga wimbo C'est trop tard Djenga. Albamu hii ilisaidia Wenge Musica kujidhihirisha kama kundi kubwa la kizazi chao. Ilipata mafanikio makubwa si tu Afrika bali pia katika Visiwa vya Antilles na Karibiani.

Mwaka wa 1994, Wenge Musica ilitoa albamu ya tano Les Anges Adorables yenye nyimbo 12. Makaba alitunga na kuimba nyimbo mbili: Tuna Tina Jack Kitshindja na Douglas Ilumbe.

Mwaka 1995, Alain alirekodi albamu yake ya kwanza ya kujitegemea iliyoitwa Pile ou Face wakati wa ziara ya Wenge Musica ya Pentagone. Nyota kadhaa wa muziki wa Zaire wakati huo, ikiwa ni pamoja na King Kester Emeneya na Dindo Yogo, walishiriki katika kurekodi albamu hiyo.

Mwaka 1996, walitoa albamu ya saba Pentagone yenye nyimbo 11 za kusisimua na Tutu Callugi na Roberto Ekokota kwa upande wa unenguaji. Albamu hiyo Alain alitunga wimbo mmoja tu: Dizoizo. Albamu hii ni ya mwisho ya Wenge Musica, kwani albamu iliyofuata Feux de l'amour iliandikwa kwa jina la JB Mpiana.

Mwezi Desemba 1997, kundi lilivunjika na Jean Bedel Mpiana, Blaise Bula na Alain Makaba wakaanzisha Wenge BCBG. Walirekodi albamu Titanic mwaka 1998.

Baadaye, wanamuziki wapya kama Jules Kibens, Rio Kazadi, Héritier Watanabe, Chai Ngenge, Alba Accompagnero, na Sunda Bass walijiunga na kundi hilo.

Makaba alihamia nchini Gabon na kuoa binti wa rais wa zamani wa Gabon, Omar Bongo Ondimba, kisha wakatalikiana na kuhamia nchini Ubelgiji.

Mwaka 2003, alirekodi albamu yake ya pili ya solo, Ya Ku Dominer.

Mwaka mmoja baadaye, alishiriki kama mpiga gitaa na mpangaji wa muziki katika albamu Mortel Combat ya ndugu Bouro Mpela na Alain Mpela.

Mwaka 2008, alifunga ndoa tena.

Mwaka 2022, alishiriki katika mradi wa kuungana tena kwa Wenge Musica uliojumuisha matukio ya kielelezo kama tamasha kwenye Uwanja wa Mashujaa wa Kinshasa tarehe 30 Juni, na tamasha la VIP kwenye Hoteli Kuu ya Kinshasa tarehe 9 Julai. Pia mwaka huo alianzisha kundi lake mwenyewe lililoitwa Al'Intime, linalomaanisha "Alain kwa Walio wa Karibu."

Diskografia

[hariri | hariri chanzo]

Albamu za kujitegemea

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]



Makala hii ni sehemu ya mradi wa kuboresha Wikipedia na Wikamusi ya Kiswahili. Unaweza kusaidia kuihariri na kuongeza habari.