Agalega

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Visiwa vya Maskarena kati ya visiwa vya Kiafrika katika Bahari Hindi

Agalega ni visiwa viwili, yaani Kisiwa cha Kaskazini na Kisiwa cha Kusini, takriban km 1,122 kaskazini kwa Morisi ambako kuna makao makuu ya Jamhuri ambayo visiwa hivyo ni sehemu yake.

Visiwa hivyo vina eneo la km² 70.

Kuna vijiji vya Vingt Cinq na La Fourche kwenye kisiwa cha kaskazini na kijiji cha Ste Rita kwenye kisiwa cha kusini.

Wenyeji wanalima mazao ya mnazi pamoja na mboga kwa matumizi yao wenyewe.

Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Agalega kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.